Haya ni maoni ya MHADHIRI MSAIDIZI WA CHUO KIKUU Bwn. Frateline - TopicsExpress



          

Haya ni maoni ya MHADHIRI MSAIDIZI WA CHUO KIKUU Bwn. Frateline Mlashani Kashaga kunihusu Ni kwa kuwa nimeweka "link" inayopingana na asemalo. Narejea...NI MHADHIRI MSAIDIZI CHUO KIKUU DSM NIMEWEKA KAMA ALIVYONIANDIKIA Kasema....... "Frateline Mlashani Kashaga Asante kwa maelezo mazuri ndugu yangu Mubelwa Bandio wewe ni mpenzi na mshabiki mkubwa wa Rais Obama nadhani kwa kuwa baba yake ni mjaluo wa Kenya hivyo unahisi Obama ni mwenzako. Maelezo yako hapo juu ni propaganda za marekani za siku nyingi. Hakuna elimu hapo juu wala mtu haitaji hata certificate ya uandishi wa habari kujua hilo. Sera ya Marekani ya mambo ya nje ni masilahi ya taifa lao kwanza , wamarekani hawana adui wa kudumu na pia hawana rafiki wa kudumu bali wao wana nmasilahi ya kudumu. Hoja yangu hapa ni moja tu, sitaki kujua Obama amefikiaje huo uamuzi wala sitaki kujua ni ushujaa gani wa kutumia presidential powers lakini ninachojua kuwa Obama ni mtu wa kustahili kupewa tuzo ya amani? Je mbona halitudanganya kuwa yeye siyo mtu wa vita?? Mtangulizi wa Rais George Bushi ni ameweka record , approval rate ya Goerge Bushi ilikuwa below 20% kwa wamerakani na ni Rais anayechukiwa sana duniani kwa sababu ni war-criminal, sasa Obama anaelekea huko huko na kupita rcord ya Bushi hivyo atakuwa war-criminal na yeye. Hivyo husipoteze muda kutetea historia ya Marekani tangia Truman maana tunajua "American economy is the war economy". Narudia sihitaji kusoma wala kujua uandishi wa Marekani, mimi nataka kujua dunia inapokea vipi ubabe wa vita wa klimasilahi wa Marekani period, pia nataka kujua ugaidi wa Obama na taifa la Marekani. Kwanza tumejifunza kwa historia ya vita ya Marekani Iraq, Libya na Afghanistani. Walimuua Gadhaffi sasa Libya imekuwa uwanja wa vita na ugaidi huwezi kuona vyombo vya magharibi vinaripoti hivyo wengi siku hizi duniani iwe China, Ulaya na baadhi ya nchi za Africa hatufuati na wala hatuamini kabisaa uandishi wa Marekani umejaa uongo na propaganda siyo taaluma ya uandishi wa habari kama unavyotaka tuamini, ni masilahi ya taifa lao hata kama itakuwa kuandika na kueneza uongo duniani. Hivyo Obama historia itamuhukumu vibaya muno na baada ya muda wake hawezi kuenjoy kama Bill Clinton anavyopendwa duniani kwa sababu Bill Clinton yeye alikuwa siyo mtu wa vita nafikiri Obama ni Rais wa kwanza wa Democratic kuwa war-monger kuliko wengine wa democratic waliotangulia. Hivyo acha ushabiki, dunia imechoka ugaidi wa kiuchumi wa Marekani, ndiyo maana wamejaa madeni makubwa hayalipiki, budget deficit kubwa, ukosefu wa ajira mkubwa hivyo wanadhani kupora nchi nyingine inaweza kuwasaidia. 5 hours ago · Like"
Posted on: Mon, 02 Sep 2013 10:32:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015