Hi ADMIN, mimi ni msichana wa miaka 22, ninaishi Dar es Salaam ila - TopicsExpress



          

Hi ADMIN, mimi ni msichana wa miaka 22, ninaishi Dar es Salaam ila nina mpenzi wangu anaishi na kufanya kazi Nairobi na tunaonana mara kwa mara. Juzi nilimtumia SMS kwamba nina ujauzito wake. Baada ya dakika kama 5 hivi akanijibu kwamba huo ujauzito si wake na kuanzia muda huo hataki mawasiliano yoyote na mimi na tuachane kabisa kama wapenzi wala tusijuane. Akaendelea kuni- SMS kwamba hawezi kunioa kwanza ujauzito si wake, sina mvuto wa kuwa mke wake, sijui kupika, sina elimu wala kipato sawa na yeye na pia hawezi kuoa mtu ambaye si kabila lake. Nilishangaa kwa kuwa siku chache zilizopita ali-propose kwamba anataka kunioa. Leo ni siku ya 3 hapokei simu wala kujibu meseji zangu. Najiuliza huyu ni mtu wa aina gani. Kiukweli sina ujauzito, nilimtumia tu SMS kama utani. Naomba upost nipate ushauri wa watu. Najua kuna wenye experience na ushauri mzuri kuhusu nini cha kufanya katika hali kama hii? Nimwambie kwamba nilikuwa namtania? Je ana upendo wa dhati na mimi kwel? ==>naombeni maoni yenu
Posted on: Tue, 09 Jul 2013 06:36:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015