Hii ndo hali gani? >Kwa kweli tajiri akifa,kiasi cha fedha za - TopicsExpress



          

Hii ndo hali gani? >Kwa kweli tajiri akifa,kiasi cha fedha za kugharamia mazishi hutofautiana kwa mbali na zile zinazotolewa kwa mazishi ya maskini ka mie... >Kiongozi mkuu anayehudhuria mazishi ya maskini labda ni chifu huku magari makubwa makubwa yatashuhudiwa yakibishana wakati wa mazishi ya bwenyenye. >Mlalahoi ka mimi,shughuli ya kunizika itafupishwa hata nizikwe saa saba unusu isivyo kawaida kwa walalahai,wakwasi wa kutajika.wao huzikwa hata baada ya saa kumi,kufuatia na wingi wa hotuba kutoka kwa wageni mashuhuri >Cha kuumiza moyo haswa ni kuwa,wakati mie mtupu nazikwa,sitazikwa barabarani huku tajiri akizikwa angani,la hasha..Sote twatiwa ardhini,tuvyonzwe na mchwa udongoni tukisubiri kufufuliwa.. Wafrika mbona twatengana?
Posted on: Mon, 04 Nov 2013 22:45:41 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015