Hikit ndio kituko cha Serikali ya Zanzibar 1. Wawakilishi - TopicsExpress



          

Hikit ndio kituko cha Serikali ya Zanzibar 1. Wawakilishi wamepewa nyongeza ya 750,000/= na ushei 2. Walimu 25,000/= minus Ushei Ukiachilia yote yanayofanywa na serikali yetu — kutimua timua dala dala pale Darajani, kuvunja nyumba za watu Bububu/Mwanyanya n.k — kupandisha bei ya umeme kwa asilimia zaidi ya 80% kuanzia Novemba 1/2013 — sasa SMZ imekuja na MPYA: 1. Imegeza mishahara ya ‘wafanyakazi’ wa SMZ wote. Wajumbe wa Bawaraza la wawakilishi watalipwa laki saba na nunsu. 2. walimu wamepewa nyongeza ya 25,000/= kama una Phdkama huna; kama umesomesha miaka mitatu, kumi, 20, mmoja n.k katika mfumo kama huo. Almuradi serikali yetu imejaa ‘big thinkers’. Nimekupeni picha halisi, sitaki kwenda sana katika details – mjue tu kuwa hiyo ndio nyongeza au SMZ wanaita ‘marekebeisho ya mishahara’. Kuna nyongeza ya siri kwa wakurugenzi na makatibu wakuu, sijui ngapi — maana ndio siri tena, almuradi wamevuna chao sihaba. Wachunguzi wa mambo — hao hao waajiriwa wanasema kuwa kama hesabu ziko sawa, wao wangaliweza kuongezwakama 100,000/ kutoka ama kasa ya wajumbe wa BLW au hao wakurugenzi na pesa itabaki nyingi kwao. Kuna walimu wamesomesha hao viongozi wa leo, na bado mshahara wao ni 100,000/ au laki moja unusu — wengine ni Master Degree, wengine na PHD holder, na wengine nai graduate lakini katika specialization fulani. – priority ni kujenga mnara wa kutimiza miaka 50 ya mapinduzi, lakini hatuna dawa, wanafunzi wanakaa chini, na ugawaji wa rasilmali [mishahara ndio huo mnauona]. Vichekesho vitupu. Ndio pale nilisema kuwa Zanzibar hatuna wawakilishi. Leo wao wameongezwa mara 100 ya kiwango cha wafanyakazi wengine,tunategemea kweli watasema nini hawa? wameshatiwa kufuli mdomoni. Nyie wenzangu wengine mtaendelea kupigwa bao tu na hadithi za katiba mpya, kwenda kibanda maiti kucheza ngoma, na mambo kama hayo ama Kidumu Chama Mapinduzi au Haki Sawa kwa Wote. Hiyo Hakiiiiiiiii…………..na hiyo ndio Kidumuuuuuuuuuu…….! Mimi sioni ajabu sana kuna haya maana mawaziri wetu ni akina Haruna Ali Suleiman, Haji Omar Kheri, Ramadhan Abdullah Shaban, Mohammed Aboud na kama hao — si wa kujua A wala B, wao ‘ulaji tu’ ndio wanaoujua. – BEI YA UMEME KUANZIA NOVEMBA 1, 2013 IMEPANDA KWA ASILIMIA 80% NA ZAIDI, LAKINI WALIOIBA NA KUHUJUMU MABILIONI WAPO PALE PALE, SASA TUNALIPA SISI WAVUJA JASHO
Posted on: Wed, 06 Nov 2013 15:19:56 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015