Hongera sana waziri kagasheki kwa mapambano dhidi ya majangili, - TopicsExpress



          

Hongera sana waziri kagasheki kwa mapambano dhidi ya majangili, pia pole sana kwa changamoto za kupigwa vita bungeni kwa kigezo cha kuua wanyama huku wakisahau askari polisi aliyepigwa risasi na majangili na kupoteza maisha papo hapo. Sijui serikali hii inataka watu wa namna gani? Au kina mulugo? Hahahahaaa maana huyu nae siyo mwenyewe. Hivi kweli amemruka katibu wake moja kwa moja? Ina maana yule katibu alikuwa anatunga? Mbona kama alikuwa anasoma? Ina maana katibu atakiwi kusema chochote kuhusu wizara? Pia pole sana profesa ( katibu) uliekubali kufanya kazi chini ya mtu uliemzidi elimu matokeo yake anakudhalisha. Mulugo ameshawahi kusema tanzania ni muungano wa tanganyika na zimbabwe leo hii profesa anaripoti kwake alafu lukuvi akapigilia msumari wa mwisho kuwa kauli ya waziri ndo kauli ya serikali hivyo basi kauli ya katibu ni yake na mke wake, profesa achana na wajinga kafundishe washakudhalilisha hao
Posted on: Tue, 05 Nov 2013 17:32:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015