Hongereni majambazi kwa kazi nzuri. Ni vibaya kusifia uhalifu ila - TopicsExpress



          

Hongereni majambazi kwa kazi nzuri. Ni vibaya kusifia uhalifu ila kwa hili nawapongeza wezi hawa kwani jeshi letu la police mwanza limekalia siasa na kusahau kaI yao. Huku jeshi la polisi limisubiria kusajiliwa kama chama baada ya kuonekana kufanya vizuri kwenye siasa kuliko kaI zake, jeshi hilo huko mwanza limetikiswa baada ya wezi kuvunja na kuiba begi na laptop mbili kutoka kituo kikuu cha jeshi hilo. Swali ni je? Ni mabegi tu na laptop ama kuna na vitu vingine kama vile silaha hatuambiwi? Je kama wezi wamefikia kuvunja na kuiba kituo cha police huku uraiani nini kinafanyika? Je nchi iko salama kwa kiasi gani?? Je kuna haja ya kuwa na jeshi hili kama ccm ikiondoka madarakani!? Maana kazi kubwa ya kikundi hiki ni kuangalia maandamano ya chadema na kuuwa raia na kama mwisho wa ccm ni 2015 waajiriwa hawa wa ccm watakuwa na kazi gani maana wezi wanatamba, madawa ya kulevia hadi kwa mama ntilie.....kazi ya watu hawa ni kufanya nini... Hakika jeshi hili linaitaji mabadiliko makubwa kwani kwa staili hii nchi haiko salama. Mungu ibariki Tanzania.
Posted on: Sat, 20 Jul 2013 01:17:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015