Hujambo! Kumekucha tayari na kikosi cha Amka na BBC kipo katika - TopicsExpress



          

Hujambo! Kumekucha tayari na kikosi cha Amka na BBC kipo katika maeneo tofauti kukupasha yanayojiri ikiwa ni pamoja na: Rais Bashar al Assad amekana kuhusika na shambulio la kemikali katika mji mkuu wa Syria Damascus. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23 warudi katika meza ya mazungumzo leo Kampala Uganda kutafuta amani. Tunakuuliza Kikwazo kipo wapi? Baadaye tutaelekea Burundi tukupashe kuhusu operesheni ya vunja vunja iliyoanza kubomoa mijengo ya haramu ya kifahari. Na leo Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto anaondoka Kenya kwenda Hague kusikiza kesi inayomkabili ya uhalifu dhidi ya binaadamu inayoanza hapo kesho. Tumekita kambi katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Nairobi. Kwa mengi zaidi jiunge nasi hewani mwendo wa saa kumi na mbili kamili kwa saa ya Afrika mashariki na pia katika mtandao bbcswahili na redio washirika. Karibu!
Posted on: Mon, 09 Sep 2013 02:19:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015