Hujambo tena! Saa kadhaa kuanzia sasa Amka na BBC, inakujia hewani - TopicsExpress



          

Hujambo tena! Saa kadhaa kuanzia sasa Amka na BBC, inakujia hewani na pia kupitia mtandao bbcswahili Leo tunamulika kwa mapana na marefu kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya naibu rais wa Kenya, William Ruto anayetuhumiwa kuhusika na ghasia zilizozuka Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Katika kipindi cha leo, tutajiunga na Peter Musembi moja kwa moja kutoka Hague Uholanzi katika mahakama ya ICC anakofuatilia kuanza kesi hiyo. Na haki ikiwa imeanza kutafutwa, miaka sita tangu kuzuka ghasia za baada ya uchaguzi mkuu Kenya, je hali ya maisha kwa waathirika wa ghasia hizo ni ipi leo? Maoni yako tunayakaribisha!
Posted on: Mon, 09 Sep 2013 22:47:47 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015