IMETOSHA Charles Ligonja J Sehemu ya 7 0714 79 77 78 ILIPOISHIA - TopicsExpress



          

IMETOSHA Charles Ligonja J Sehemu ya 7 0714 79 77 78 ILIPOISHIA “Unaniua mke wangu” “Kufa kabisa,wewe ondoka hapa”Yule msichana alitoka baada ya kumwaga kojo la nguvu kwa mshituko alioupata kwa kile alichokiona……FUNGUA MACHO,SONGA MBELE……. Alipotoka yule msichana nami nikaamini ni wakati wa kugombana na mume wangu na kwa imani ambayo ameijenga kwangu kwamba mara nyingi akiwa na kosa huwa mpole lakini siku hiyo mambo yalikuwa tofauti,Freddie alisimama pale chini kama umeme na kunivamia,alinipiga sana huku akinilaumu kwanini nakuja bila kutoa taarifa. “Nitoe taarifa wakati nakuja kwangu” “Unajifanya kiburi sio,ngoja nikuoneshe leo” Freddie aliendelea kunipiga pale chini na kila nilipojaribu kujinasua sikuweza kwani anasema kwa vile nimepanga kumvunjia heshima basi bora anipige mpaka atosheke na kipigo kifanane na aibu ambayo nimemtia. Nilioona hali mbaya niliamua kutumia nguvu ili asije akaniua kwani alikuwa na kila na dalili ya kuniua,alinikaba sana na nilipofanikiwa kumtoka nilikimbia sana na sikurudi mpaka siku ya pili yake. Nilipofika pale nyumbani asubuhi nikaingia ndani moja kwa moja na kukutana na maneno ya kashfa toka kwa mume wangu,sikuamini angekuwa vile,alionesha hasira ya dhahiri,hakupenda nilichokifanya jana yake. “Umekuja,umekuja tena kunivunjia heshima,ondoka mama nisije nikakuua” “Unasemaje,unayoyanfanya unaona yako sawa? “Kimya unadhani yote unayoyafanya huko nzega suyajui,mimi nina shahada kama wewe lakini mshahara wangu haufiki hata laki tano,wewe unalipwa milioni moja na nusu,we endelea na huyo bwana wako”Freddie aliendelea kuongea aliyoweza kwa kifupi nilipigwa na butwaa kwani kiukweli mishahara ya migodini iko juu kidogo ingawa kwa pesa ambayo wawekezaji wanaipata ni tofauti na mishahara yetu,wanapata faida kubwa sana,wengi walipenda kufanya kazi migodini kutokana na pesa iliyokuwa ikilipwa,kumbe kitu hicho kwa mume wangu ni tofauti alijua nina mwanaume ambae ananitia kiburi na kutokana na imani hiyo basi nae akaamua kufanya yake. “Freddie kama uzinzi hujaanza leo,mshahara wangu isiwe kisingizio cha wewe kufanya unayofanya” “Nikwambie kitu kimoja umerudi safari hii ujue hurudi tena kazini,siwezi mimi” “Unasemaje?!kwa kipi hasa cha kunibakisha hapa?”Lilikuwa kosa kubwa kusema vile kwani kipigo kilianza upya akisisitiza kwamba sina heshima kwa sababu tu nimemzidi kipato sasa ili niwe na heshima basi niache kazi na yeye yuko tayari kunihudumia kitu ambacho nilikataa katakata,sikuwa tayari kuacha kazi ambayo ina maslahi kwangu,kazi yangu imechangia kuweza kumaliza ile nyumba,eti niache kazi kwasababu yake!!! “Kwahiyo kiburi sio?” “Hilo unalofikiri kama unaona uko sahihi basi amua lingine lakini kuacha kazi haiwezekani” Niliongea kwa kujiamini mtoto wa kike wakati huo Freddie akiwa juu yangu akiendelea kinifinya masikioni ili nikubaliana na matakwa yake,sikuwa tayari kurudi kwenye zile shida ambazo kwa kiasi fulani zimeanza kupungua na kikubwa nilichokuwa nataka ni nyumba kwanza badae kununua gari ambalo nilishaagiza,leo niache kazi nisubiri mshahara wa mwalimu!! Siku hiyo ilipita bila maelewano na alipoona nimeshikia msimamo wangu aliamua kuondoka na kuniacha nyumbani nikiamini atarudi badae na mawazo mengine kumbe sivyo,alikokuwa akatuma ujumbe mfupi wa maneno kama nimebadili uamuzi wangu ama lah,nikamwambia hapana.alianza kutuma meseji za matusi aliandika kila aliona linamjia kichwani mwake,alinitukana mimi alipoona haitoshi aliamua kuhamia kwenye familia yangu,alianza kumtukana mama na baba,badae kaka zangu na kuhamia hata kwa marehemu wa ukoo wetu,sijui alikuwa anawaza nini kwa vile alivyokuwa akiandika na kutuma kwangu,mwanaume niliyempenda kwa dhati ya moyo wangu leo ananiona sina maana,kwanini basi asinitukane mimi peke yangu,wazazi wangu wana kosa gani mpaka yawafike yote hayo ingawa walikuwa hawajui kama wanatukanwa na mkwe wao. “Festo una muda tuongee?” Festo alikuwa kimbilio langu popote nikiwa na tatizo basi yeye alikuwa wa kwanza kumpigia nae alikuwa akinishauri vizuri lakini pia kumbuka ndugu msomaji hapo nyuma nilipokuwa nikiishiwa na mume wangu Freddie,Festo alikuwa kimbilio langu,sina cha kumlipa zaidi ya kumwombea apate mke mwema.Aliniambia ana muda nami nikamwambia yote yalijiri. “Chezea mapenzi Annie lakini kazi ni kitu kingine,ona vijana wanavyosaga soli za viatu,mpaka kiatu kinakaa upande,angalia machinga wanavyotembea bila kupata kitu siku nzima,leo uache kazi ambayo inakulipa vizuri kisa mapenzi….lakini kila mtu na namna apendavyo katika mapenzi,uamuzi ni wako” ‘Siwezi kufanya maamuzi ya kipuuzi,bora tuachane” ‘Fanya maamuzi sahihi rafiki yangu” “Kweli,bora tuachane” “Uachane na nani,ndo mpango wako sio,haya niambie ulikuwa unaongea na nani muda wote au ndo huyo anaekupa kiburi” “Niache bwana,naongea na nani naongea na nani,naongea na mwanaume” “Si nilisema,kuna mtu anakutia kiburi sio bure,nipe simu” Ugomvi ulianza upya Freddie alikuwa anataka simu ili ajue niliyekuwa naongea nae,haikuwa rahisi kuachia simu yangu kwani niliamini atampigia simu na kumtukana kitu ambacho sikutaka kitokee kwa rafiki yangu kipenzi lakini bahati mbaya jitihada zangu hazikuzaa matunda,Freddie alinizidi nguvu na kuchukua simu na alipoiangalia na kuona namba ya mwisho kupigwa aliamua kuipiga ana ilipopokelewa kabla ya salamu wala nini alianza kumtukana Festo wangu,alimtukana sana,niliumia sana kwani nilikumbuka mengi ambayo Festo ameyafanya hapo nyuma kumsaidia yeye hasa kipindi kile alipowekwa rumande leo amtukane. “Unajua mtu unaemtukana ndiye aliyenipa pesa ambazo nilitumia kukutoa rumande” “Mimi hanisaidii chochote,ngoja nimtukane akome,pumbavu” Nilijisikia aibu sana kwa yale aliyokuwa akiyafanya mume wangu,sijui kama Festo atapokea simu yangu na hata kama nitampigia nitamwambia nini anielewa kwani kama matusi tayari ametukanwa tena na mtu ambae alimsidia hapo nyuma. “We mwanamke tatizo lako umalaya,eti nisimtukane,kwasababu unamvul**a kama mimi uniafanyiavyo?Haya nimeshamtukana sasa fanya” Sina uhakika kama mume wangu yuko sawa,kwanini anafanya mambo ya ajabu kiasi kile kama yuko timamu!? Siku hiyo kila mtu alilala chumba chake,sikuwa na hamu na mume wangu kama siku zingine nilipokuwa nikitoka likizo ambazo tulikuwa tukifurahia penzi letu,lakini baada ya kufika na kuona yuko na mwanamke mwingine mzuka ulipotea kabisa,sikutaka kuwa faragha na mume wangu. Kwa kifupi nilitamani kuondoka usiku huo niende nikalale gesti kama jana lakini badae nilipopata wazo la kulala chumba kingine niliamua kufanya hivyo.Usiku wa manane nilipitiwa na usingizi nilisikia mlango ukigongwa kwa nje na niliposikia kwa umakini kumbe alikuwa Freddie akitaka nimfungulie tualale wote,jamani huyu mwanaume hatosheki jana alikuwa na mwanamke mwingine leo anataka kuja kufanya hayo hayo na mimi,sifungui sasa,mlango uligongwa lakini niliamua kutofungua na ndicho kilichotokea kwani sikufungua na alipochoka aliondoka na kuingia chumbani kwake mpaka asubuhi. ************************************************************** Freddie alikuwa wa ajabu sana kwani tulipoamka asubuhi eti alikuja na kunilaumu kwanini jana sikufungua mlango wakati alikuwa arnemiss na alitaka kuwa karibu na mimi na hata kulala wote,tuenjoy!! “Nani kakwambia mwanaume anaweza kukaa wiki nzima bila kupata chakula ya roho?” “Mbona kumekucha sasa” “Nimeumia sana usiku ulipogoma kufungua mlango kwani treni lilishawaka,imemchukua muda sana kulizima”Nilitamani kucheka kwa sauti lakini kutokana na hasira nilizokuwa nazo hasa kitendo cha kumtukana Festo,nilipokumbuka hilo hasira zangu zilirudi upya,nilimwangalia kwa hasir sana na alipoamua kuniomba msamaha. “Naomba yaishe” Simu yangu iliita na nilipoiangalia alikuwa Festo,nikipokea nitamwambia nini anielewe,je hatawaza kama nilimpa simu mume wangu amtukane,jamani Annie afanye nini?Nisipopokea nalo ni tatizo wakati naendelea kuwaza simu ilikatika,haukupita muda mrefu simu yangu iliita tena,alikuwa Festo lakini sikupokea. “Kuna issue ya kazi,nipigie au pokea simu nikupe dili ili mumeo aachane na ualimu”Iliimgia meseji kwenye simu yangu,alikuwa Festo akinitaka nipokee simu anipe dili,nilitamani kumpigia lakini moyo ulisita,mara ujumbe mwingine. “Kama una simu ya mkeo naomba umwambie kuna dili bomba”Masikini Festo ingawa alitukanwa jana lakini alikuwa tayari kutimiza ahadi aliyoiweka hapo nyuma kwamba kama siku akipata sehemu inayotaka mtu kama Freddie basi atamuunganishia.Niliamua kumpigia. “Mambo Annie!” “Nisamehe Festo” “Achana na hayo,ni hivi kuna asasi moja ya kiraia inataka mtu wa project management na kwa vigezo watakavyo naamini mumeo atafaa” “Ataelewa kweli” “Kwanini asielewe,mwambie atume CV zake haraka,kuna donge nono..jamaa wageni wanalipa milioni tatu kwa mwezi na gari anapewa” “Acha utani,si atalala kiwandani huyu mtu kwani za bar hazitamtosha” “Acha utani,mi nimelamba ubwana fedha makao makuu” “Yaani mtakuwa ofisi moja?” Maswali yalikuwa mengi toka kwangu kitu kilichopelekea Festo akate simu kwani alikuwa hapendi kuongea na simu muda mrefu,alikuwa akiumwa kichwa akama ataongea muda mrefu na alijaribu kutuimia ear phone lakini hazikumsidia hivyo alikuwa akitumia simu kwenye kutuma ujumbe mfupi wa maneno. Niliwaza ni namna gani nitaanza kumpa huo ujumbe mume wangu kwani sikuwa na imani kama atakubali,sikuwa na namna baada ya kuwaza sana niliamua kumwambia hilo,hakuamini na kitu cha kwanza aliomba nimwombee msamaha kwa Festo na ikibidi basi waonane na amwombe msamaha kwa alichokifanya jana,alikuwa anamuwazia voibaya kumbe mwenzake hakuwa na mawazi mabaya zidi yake,alipenda kuona nae anafanikiwa kwenye maisha yake hasa kwa kupata kazi nzuri ambayo itamlipa kwani aliamini kwenye ualimu hakuna atakachopata zaidi ya madeni. Annie alimpigia simu Festo nae akasema hayo kwa muda huo sio muhimu isipokuwa la muhimu ni kutuma hizo CV ili apate kazi na kweli alituma.ITAENDELEA!!Je atapata hiyo kazi?Fuatilia siku nyingine.
Posted on: Sat, 29 Jun 2013 11:06:24 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015