Ibara ya 30 ya rasimu inatuhusu wanahabari,naiweka hapa ili - TopicsExpress



          

Ibara ya 30 ya rasimu inatuhusu wanahabari,naiweka hapa ili muione,tunashukuru sasa rasimu imetaja uhuru wa vyombo vya habari(30)2,lakini rasimu inataka kutupeleka kulekule tunapolalamikia kwenye National security act,newspaper act,prison act,baada ya kuweka kipengele kibaya kwa uhuru wa wanahabari,kipengele hicho ni Ibara ya 30(4),unaweza kupitia kama nilivyokiweka,ni vizuri wadau wote wa habari tupige kelele ili kifungu hicho kitoke,kikibaki uhuru tunaoulilia tutakuwa hatujaupata,kamati ya Jaji warioba imetuwekea mtego,tuutegue kabla haujawa sheria............soma ibara hii hapa chini... 30.-(1) Kila mtu anao uhuru wa- (a) kutafuta, kupata na kutumia habari na taarifa na kusambaza taarifa hizo; na (b) kuanzisha vyombo vya habari na njia nyingine za upashanaji wa habari bila kujali mipaka ya nchi. (2) Vyombo vya habari vitakuwa huru na vile vile vitakuwa na: (a)haki ya kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa wanazopata; (b)wajibu wa: (i) kusambaza habari na taarifa kwa wananchi; na (ii) kuheshimu na kulinda utu, heshima, uhuru na staha ya wananchi dhidi ya habari na taarifa wanazozitumia, wanazozitayarisha na kuzisambaza. (3) Serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na watu binafsi watakuwa na wajibu wa kutoa habari kwa umma juu ya shughuli na utekelezaji wa shughuli zao. (4) Masharti ya Ibara hii yatalazimika kuzingatia masharti ya sheria ya nchi itakayotungwa kwa ajili hiyo na kwa madhumuni ya kulinda usalama wa Taifa, amani, maadili ya umma, haki, staha na uhuru wa watu wengine.
Posted on: Tue, 23 Jul 2013 18:06:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015