Ibara ya 8. Ibara ndogo ya (1), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - TopicsExpress



          

Ibara ya 8. Ibara ndogo ya (1), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo - (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi; (c) Serikali itawajibika kwa wananchi; (d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii. Ibara ndogo ya (2), Muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, au wa chochote kati ya vyombo vyake na uendeshaji wa shughuli zake, utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na haja ya kukuza umoja wa kitaifa na kudumisha heshima ya Taifa. https://play.google/store/apps/details?id=tz.co.yetu.katiba.katiba
Posted on: Tue, 25 Jun 2013 16:11:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015