JE KUNA UKWELI NDANI YA - TopicsExpress



          

JE KUNA UKWELI NDANI YA HILIIIII????????????????????? NIMELIKUTA MAHALI EMU TUJADILI Mzee Edwin Mtei ni muasisi na mmiliki wa Chadema. Godbless Lema ni kijana wa Mtei. Freeman Mbowe ni mkwe mpwa wa Mtei. Yaani huyu ana ukaribu na Mtei kama mme wa binti yake, lakini pia anamuita Mtei mjomba. Godbless Lema na Mbowe ni marafiki wa karibu na ni binamu wa mbali - 6th cousins. Uwepo wa Lema na Mbowe kwenye nafasi za juu za maamuzi ndani ya Chadema ndio kitu pekee kinachomfanya Mtei atulie shambani kwake Tengeru bila hofu. Anajua Chadema bado iko mikononi mwake. Maamuzi yote yanafanyika Tengeru halafu vikao vinakaa kuyapitisha tu. Baada ya kijana wa Mtei, Godbless Lema kumshambulia mitandaoni mbunge mashuhuri kuliko wote Tanzania - Zitto Kabwe, ililazimika ajibiwe. Baada ya Lema kujibiwa, ikaonekana hana hoja na momentum ikawa upande wa Zitto. Jambo hili limemsononesha sana Mtei na kumtia hasira. Pia imempa Mtei hofu kuu kuona kwamba upo uwezekano wa wanachama kukichukua chama kutoka mikononi mwake! Kutoka Tengeru chadema ingepelekwa matawini. Jambo hili Mtei ameshindwa kulivumilia. Zitto alianza kushutumiwa na Chadema alipotangaza kugombea uenyekitu katika uchaguzi uliopita. Kabla ya hapo alionekana ni mtumishi mwema, alisifiwa na kupigiwa makofi anapoongea. Kosa lake lilikuwa kuhatarisha nafasi ya mkwe mpwa wa Mtei, Mbowe. Zitto ameadhibiwa kwa kupinga maneno ya Lema kwenye mitandao. Pamoja na kwamba Zitto ni kiongozi wa Lema, lakini Lema ni more insider than Zitto in todays Chadema. Kitila Mkumbo alitumiwa na Mzee Mtei kubadilisha matokeo ya viti maalum ili mabinti wa Mtei, Ndesamburo na wengine wanaowataka wapate Ubunge. Yeye Kitila hakuingiza mtu yeyote wake. Kura zilizopigwa na wajumbe zikafutwa na wabunge wakateuliea kwa kufuata vigezo vilivyotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu na Kitila Mkumbo. Alichotaka Mtei kikafanikiwa. Kosa la Kitila ni kumsema hadharani Henry Kilewo kwa kusambaza waraka wa majungu dhidi yake. Henry Kilewo alishirikiana na viongozi wengine wa Chadema kusambaza waraka wenye lengo la kumchafua Zitto na kutaja jina la Kitila. Waraka huu ulitolewa baada ya Lema kushindwa kwa hoja na Zitto. It is therefore reasonable to presume kwamba Lema anahusika na waraka huu. Mzee Mtei alitaka Kitila akae kimya ili Zitto abaki peke yake. Lakini Kitila aliandika mitandaoni kuwa Zitto ni rafiki yake wa siku nyingi na kama mtu mzima hawezi kuchaguliwa rafiki. Jambo hili limemsononesha Mtei na kuhatarisha nguvu zake juu ya Kitila. Lema na Mbowe hawawezi kupinga jambo lolote analotaka Mtei. Ndio maana hata pale Mtei alipitoa unpopular comment kuhusu composition ya tume ya katiba, Mbowe aligoma kama mwenyekiti kudenounce kauli ya Mtei. Akamtuma Mnyika atoe tamko la kiujumlajumla kuwa Mtei ana haki ya kutoa maoni yake binafsi hata kama ni ya kibaguzi na yanahatarisha umoja wa kitaifa. Tukumbushane tu kuwa Mtei alikuwa kijana msomi wakati harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika zikiendelea. Mtei aliombwa mara kadhaa kusaidia katika harakati hizo lakini alikataa. Mtei alikuwa mtumishi mtiifu wa wakoloni. Uhuru ulipopatikana, Mtei aliombwa tena kushiriki ujenzi wa Taifa. This time Mtei alikubali kwa masharti kwamba alipwe mshahara sawa na waliokuwa wanalipwa wakoloni. Nyerere alikubali kwa shingo upande kwa vile hakukuwa na mtanzania mwingine aliyekuwa na elimu ya uchumi kama Mtei. Mtei akawa analipwa mshahara mkubwa kuliko Rais Nyerere. Baada ya vita vya Uganda, uchumi wetu ulitetereka. Wananchi wakatakiwa kufunga mikanda (kuvumilia hali ngumu). Mtei hakutaka kuvumilia hali ngumu. Akamshauri Nyerere serikali ichukue mikopo mikubwa IMF na World Bank kwa masharti yao. Nyerere alikataa ukoloni huo mamboleo. Mtei akasusa kuwatumikia watanzania bila malipo manono. Akajiuzuru... Ndio maana kijana wa Mtei, Lema hayuko tayari kuachia au kupunguza posho ya vikao. Hiyo ni falsafa aliyofundishwa na Mtei. Zitto anaadhibiwa kwa kupinga falsafa ya Mtei hadharani. Lema ni kifaranga tu kilicho juu ya chungu lakini chini ya chungu hicho yuko Mtei. Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...
Posted on: Sat, 23 Nov 2013 17:58:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015