"JE NI SAWA?"Ndugu zangu watanzania,kuna jambo nataka tusaidiane - TopicsExpress



          

"JE NI SAWA?"Ndugu zangu watanzania,kuna jambo nataka tusaidiane mawazo,jambo lenyewe ni kitendo cha mwanaume kukutana na mwanamke na kumwambia nakupenda nataka kukuoa kisha akataka kushiriki nae tendo la ndoa kabla ya ndoa,binafsi kwanza wanaume tuwe wakweli tutofautishe kati ya kupenda na kutamani,kwani ukimuoa unaemtamani utajisababishia matatizo,ni vigumu kukaa kindoa na unaemtamani,na ukisema unampenda basi iwe kweli ili mwanamke asije akamkabidhi moyo wake kwa 100% kwa asiyempenda ataumia sana,kisha suala la kushiriki tendo kabla ya ndoa linamuathiri sana mwanamke kwani wengi wao baada ya tendo hawaolewi tena wanaharibiwa mastakbali wa maisha yao,usia wangu kwa wakinadada kwanza ujione ni watu muhimu sana ktk jamii,msijirahisishe,mjiamini na muwe na msimamo,yeyote atakaekufuata na kukwambia nakupenda nahitaji kukuoa nawe ukampenda mwambie kwa kulinda heshima yako sawa lakini fuata taratibu,usimpe,kuna watu wanasema mpaka waonje,kwani hii chai?uonje nini? haya ni mawazo yangu,nahitaji mawazo yako.
Posted on: Sat, 03 Aug 2013 11:32:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015