JITIMU LIPI LI KALI MANICHESTA KUKABILI Nawapeni jambo hili, - TopicsExpress



          

JITIMU LIPI LI KALI MANICHESTA KUKABILI Nawapeni jambo hili, kujuzeni ya ukweli, Barani kwenye utuli, Manichesta yawa kuli, Kambumbuni wa jabali, zote Timu kukabili Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili Ulayani wa fahali, Moyesi kuwafadhili, Asenali Livapuli, zote timu kuzifeli, Kombe nyingi za awali, uropani sizo mbili, Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili Wachezaji bei ghali, kunoleshea makali, Ushindi ndo wanajali, ugani kuwa kamili, Moja unusu lisali, mahasimu kudhalili, Jitimu lipi li Kali, Manichesta kukabili Guu mosi guu mbili, kungoa nanga ya mbali, Changamoto kutobali, safarini kutofeli, Hata chungu pilipili, tameza jaziri hili, Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili Wawili sio fahali, zizini kpewa himili, Sheria ya futiboli, washindani ni wawili, Manichesta si tofali, majabali wakatili, Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili Naombea ya jalali, Oltrafodi au mbali, Ya Mali pia ya hali, isiwe ndumakuwili, Kupasi iwe kauli, ubingwani futiboli, Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili Wa chumvi au asali, ukweli haubadili, Moja natowa kauli, maheitas mukubali, Shuhubiri ni ukweli, domo halistahimili, Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili Twafunga zetu faili, mapepo yalo bahili, Karibuni Jumapili, tuwalishe kwa ugali, Ingawa sisi hatuli, twawapa nyingi magoli, Jitimu lipi li kali, Manichesta kukabili
Posted on: Fri, 11 Oct 2013 17:12:46 +0000

Trending Topics



" style="min-height:30px;">
Little Scotty McMillan is dead. Over a three day period ... he was

Recently Viewed Topics




© 2015