Jamaa kapoteza mali zote na akawa maskini wa kutupwa kwa sababu ya - TopicsExpress



          

Jamaa kapoteza mali zote na akawa maskini wa kutupwa kwa sababu ya ulevi. Siku moja asubuhi akawa anapita karibu na jalala akaona chupa tupu za bia. Akaishika ya kwanza akaipasua: kwa sababu yako nimeachana na mke wangu. Akaichukua ya pili akaipasua: kwa sababu yako nimeshindwa kusomesha wanangu. Akaichukua ya tatu akaipasua kwa hasira: kwa sababu yako nimefukuzwa kazi. Akaishika ya nne nayo akaipasua: kwa sababu yako nimeuza mali zangu zote hadi nimefilisika. Akaichukua ya nne ila akakuta imejaa bia na bado haijafunguliwa akasema: we kaa pembeni kwanza, huu ugomvi hata haukuhusu, tutaongea baadaye ila ole wako na wewe unifanye kama walivyonifanyia wenzako.
Posted on: Wed, 17 Jul 2013 13:26:40 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015