Jamaa mmoja dereva wa pikipiki asema alipigiwa simu na mkewe - TopicsExpress



          

Jamaa mmoja dereva wa pikipiki asema alipigiwa simu na mkewe kwamba nyumbani kulikua na mgeni aliyetumwa kwake.Jamaa alifika na kweli akapata mwanamume ambaye mkewe alimtambulisha kama kakake mkubwa kutoka mji wao wa pili ambao huyu Jamaa hakuwa amewahi fika yeye alijua tu kule anakotoka mkewe.shemegiye alisema ametumwa shilingi 10,000 au 8,000 za kumpelekea babake mkewe hospitali kwa kuwa alikua mgonjwa sana na iwapo hana basi arudi na dadake kwenda kuthibitisha kwamba hakupata hela kama alivyotumwa.Jamaa ilibidi aache mkewe aenda na kuahidi kumfuata keshoye akiwa amewahi chochote.Jamaa alijitolea kuwapeleka lakini Yule shemegiye akataka wapelekwe Malindi mjini alikodai anafanya kazi kwa hoteli flani kabla ya kumfikisha dadake nyumbani.Kesho ilipofika Jamaa alipiga simu kwa kina bibi yake na akaambiwa mkwewe hakuwa mgonjwa wala bibiake hakuwa huko,mji wa pili pia hawaujui.alijaribu kupiga ile nambari aliyopigiwa na mkewe ikawa ni mteja,akaamua kuenda ile hoteli aliyodai shemegiye anafanyakazi na akaambiwa hakuna mtu kama yeye hapo.Sasa hajui aliko mkewe pamoja na Yule Jamaa mwengine ambaye anashuku alikua mpango wa kando wa mkewe.Afanyeje?Voroni ukiwa na Dama na Kalambua.
Posted on: Fri, 21 Jun 2013 03:23:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015