Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Matukio - TopicsExpress



          

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Matukio Matatu Tofauti Likiwemo la Selena Mwinuka Mkazi wa Mtaa wa Kibena Mjini Njombe Aliyefariki Akiwa Chumbani Kwake Huku Likimshikilia William Kaunda Mkazi wa Zambia Kwa Kusababisha Kifo cha Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Katika Shule ya Sekondari Luduga. Akizungumza na Mwandishi wa Kituo Hiuki Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani Amesema Matukio Hayo Yametokea Novemba Kumi Mwaka Huu Katika Maeneo Tofauti. Cue....Ngonyani Nov 11 Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Tukio Lingine Limetokea Barabara Kuu ya Mbeya-Makambako Ambapo Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Katika Shule ya Sekondari Luduga Fanuel Mhanzi Amefariki Baada ya Kugongwa na Gari Lenye Namba za Usajili ACV.4199 Toyota Corolla Mali ya Seventy Seventy Five Car Hire Investment ya Ndola Zambia . Amesema Gari Hilo Lililokuwa Likiendeshwa na William Kaunda Mkazi wa Zambia Lilimgonga Mwanafunzi Huyo Akiwa Anaendesha Baiskeli na Kumsababishia Kifo Chake Papo Hapo.
Posted on: Tue, 12 Nov 2013 16:10:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015