KAMA HAUKUJUA BASI JUA: Kinyonga ana sifa hizi ambazo pengine - TopicsExpress



          

KAMA HAUKUJUA BASI JUA: Kinyonga ana sifa hizi ambazo pengine hukujua:- 1. Jina lake linatokana na maneno mawili ya kigiriki CHAMAI-ARDHI na LEON-SIMBA. Hivyo linamaana ya SIMBA WA ARDHINI. 2. Kinyonga anaweza kuangalia pande mbili tofauti kwa wakati mmoja. Yaani anaweza kuangalia mbele kwa jicho moja , halafu nyuma kwa jicho lingine ! Macho yake yana uwezo wa kuzunguka! 3. Hata hivyo kinyonga hawana masikio. 4. Anaweza kubadilisha rangi yake ndani ya sekunde ishirini! 5. Ulimi wa kinyonga ni mrefu kwa wastani wa mara moja na nusu au mara mbili ya kiwili wili chake. 6. Na ulimi wa kinyonga ndio nyenzo yake kubwa katika kula, hutumia kukamata wadudu, ulimi huo huweza kugeuka kuwa kama kikombe na mdudu kudumbukia humo. --Chanzo: findfast.org na bestfanfacts
Posted on: Fri, 22 Nov 2013 14:54:37 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015