KARIBU AFRIKA RAIS OBAMA Katika hali isiyo ya kificho na - TopicsExpress



          

KARIBU AFRIKA RAIS OBAMA Katika hali isiyo ya kificho na kububujikwa na furaha waafrika wate duniani ni pale walipoona mwafrika wa kwanza mweusi tena mwenye asili ya Afrika, Kenya anatawazwa kuwa rais wa taifa kubwa lenye nguvu duniani Amerika, ndugu yetu mpendwa rais Barrack Hussein Obama. Waafrika wengi wangefurahi zaidi kama uongozi wa Obama ungeshuhudiwa na Dk. Martin Luther King Jnr, baba yake Obama, Mama yake, Tom Mboya aliye kuwa rafiki mkubwa wa Matin Luther King aliyepata kuwa msemaji mkuu wa kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya Wanegro kwenye mkutano uliosheni watu mwaka 1959 pale Washington, Nkwame Nkuruma, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Samora Machel na hata Patrice Lumumba aliyeonja uwaziri mkuu ndani ya miezi miwili na kuuawa kikatili na Wabelgiji na wasaliti wachache waafrika. Kwa hawa wote waliolala mauti tunawaombea Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi. Amina Hii inatudhihirishia kuwa ndoto za Martin Luther King na wengine wote kuwa mwafrika siku moja angejitawala na kutawala nchi kama ya amerika imetimizwa. Muhimu kumtia moyo kwani anatawala nchi yenye changamoto nyingi, Obama amewafurahisha watu wengi wa bara la Afrika anapoamua kutembelea nyumbani kwao Afrika Mashariki, hajaenda Kenya siyo kwa sababu zake mwenyewe ila ni kwa utashi wa ikulu ya White House kutokana na watawala wote wawili wa Kenya yaani rais na makamu wake kutuhumia kwa mauaji ya alahiki mwaka 2007 ila naamini mara tu baada ya urais wake ataweza kwenda Kenya hasa kijijini kwao kama Obama na wala siyo kama rais wa Amerika. Aluta Continuous! Mungu mbariki Obama, wabariki watoto wa Afrika, bariki bara la Afrika.
Posted on: Thu, 27 Jun 2013 07:28:48 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015