KUHITILAFIANA KATI YA FATUMAH BINT RASULULLAH NA SAYYDINA - TopicsExpress



          

KUHITILAFIANA KATI YA FATUMAH BINT RASULULLAH NA SAYYDINA ABUBAKAR Muda mfupi baada ya Abubakar kujinyakulia madaraka ya kuongoza Uislamu pale Saqifat Bani Saidah, Bi Fatumah alikwenda kwa Maanswar kuwaomba watekeleze maagizo ya Mtume kwa kumpatia baia Ally ibn Abi Talib, lakini Maanswar wakamwambia tayari tumekwishampa Abubakar na kwamba kama angekwenda mapema wasingempatia baia mtu yeyote isipokuwa Ally. Kwa hili Imam Ally anasema, “hivi kweli ni busara nimuache Mjumbe wa Allah nyumbani kwake bila kumzika ili tu nitoke kuja kugombana na watu juu ya cheo changu?” Fatumah naye akasema, “alichofanya Abul-Hassan ndicho kilichompasa kukifanya, na wao wamefanya jambo ambalo Mwenyezi Mungu atawauliza na atawalipa (kwa tendo la kupora madaraka). Tazama: tarikh Al-Khulafaa cha ibn Qutaibah J. 1 uk. 19 na Sharh Nahjul Balagha cha ibn Abil Hadid (Baiatu Abubakar). Kwa dhuluma aliyoifanya Abubakar na wenziwe dhidi ya Ahlulbayt wa Mtume, Bi Fatumah alimchukia Abubakar kiasi kwamba alipokufa aliagiza Abubakar asihudhurie mazishi yake na wala asijue kaburi lake lilipo. Hivyo Mmewe alimzika bibi huyo usiku na mpaka leo hakuna kauli moja inayoonesha kaburi la bi Fatumah lilipo. Tazama: sahihi Bukhar J. 3 uk 36, na Sahih Muslim J. 2 uk. 72 Hivyo utagundua kuwa bibi huyo mtukufu ambaye Mtume alimtangaza kuwa mmoja wa wanawake bora zaidi ulimwenguni akiwa kati ya wanawake bora wane tu, alihitaji mazishi yake liwe fundisho kwa waislamu ili wajiulize kuna kitu gani kilitokea baina yake na watawala wa zama hizo. Na kwa hakika tumekwisha jiuliza na kujuwa hujuma uliza fanyiwa ewe mama wa Makhalifa na maimamu watukufu. il y a 20 minutes
Posted on: Thu, 29 Aug 2013 18:04:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015