KUTOA SADAKA SADAKA NI NINI? Sadaka ni aina ya matoleo - TopicsExpress



          

KUTOA SADAKA SADAKA NI NINI? Sadaka ni aina ya matoleo yanayotolewa na mwanadamu kwa maana ya kumrudishia MUNGU wake shukrani. Tena ni agizo la MUNGU mwenyewekwa mwanadamu kuwa atoe kwa kupenda. Kutoka 25:1-3 AINA ZA SADAKA Ziko aina nyingi za sadaka ambazo MUNGU ameagiza kutoa kwake nazo ni:- 1. Sadaka ya kawaida. Hii inaitwa shukrani ambayo mwanadamu anatoa kumshukuru MUNGU kwa ulinzi, amani, upendo, kuongozwa na kutunzwa naye kwa mambo mbalimbali kwa wiki nzima, ambapo huja Jumapili kutoa sadaka. 2. Zaka au fungu la kumi. Hii ni lazima kutoa tena kamilifu. Hii hutolewa kanisani kwa Kuhani. Malaki 3:10 3. Nadhiri au ahadi. Soma Kumb. 23:21-23 4. Shukrani kwa yale uliyotendewa naye. Mfano, kupona katika ugonjwa, kupata kazi, kufunga ndoa, nk. Zaburi 136:1. 5. Dhabihu. Hii mara nyingi MUNGU husema nawe moja kwa moja. Mwanzo 22:1-3 6. Malimbuko. Kila kitu cha kwanza, mfano, mshahara wako wa kwanza wote ni sadaka kwa MUNGU, toka shambani mazao ua mifugo, biashara ile faida ya mapato ya kwanza ni mali ya MUNGU. Nehemia 12:44, Kumb. 26:1-2, 10-11, 2Nyakati 31:4 - 6. 7.Mavuno. sadaka hii hutolewa mara moja toka katika mshahara wako, shambani, biahsara zako. Kumb. 26:1-2, 10-11 8. Sadaka ya dhambi 9. Sadaka ya upatanisho. Sadaka hizi mbili na. 8 na na. 9, kwa sasa hazipo kwa sababu BWANA YESU ametulipia deni la dhambi na ametuatanisha na MUNGU kwa njia ya mauti yake pale msalabani. Soma Warumi 5:9-10, Walawi 17:11. Kwa kufuata Biblia, hizi ndizo tunaziita sadaka ambazo kila Mkristo anapaswa kuzijua na kutoa kwa wakati. TUNATOA WAPI SADAKA? Sadaka kama sadaka tunatoa nyumbani mwa BWANA maana ndipo mahali sahihi pa kupeleka sadaka yako kwa maana hapo ndipo tunakutana na BWANA. Kumb. 12:5-7. Wakati wa kupeleka na kutoa sadaka yako hakikisha kwamba sadaka yako inaambatana na maombi ya uhitaji wako au shukrani zako. KWANINI TUNATOA SADAKA? 1. Tunatoa sadaka kama agizo la MUNGU mwenyewe. Kumb. 8:6, Kutoka 25:1-2 2. Tunatoa sadaka kuonyesha utii kwa MUNGU wetu wa upendo. Kumb.28:1, Isaya 43:4 FAIDA YA KUTOA SADAKA Ziko faida nyingi azipatazo mwanadamu kwa kutii na kuwa mwaminifu katika kutoa;- baraka, ulinzi, afya, nk. Malaki 3:10, Kumb. 28:1-4, 2Nyakati 31:10b, Kumb. 28:7-10 HASARA ZA KUTOKUTOA SADAKA MUNGU anaruhusu kila aina ya ubaya ya madhara yanayokupata wewe, mf. magonjwa. MUNGU anaondoa ulinzi kwako na katika maeneo mbalimbali yanayokuhusu, mf. kazini, kwa watoto, mali zako, nk. Kumb. 28:20, 45-48 BWANA atusaidie katika kukumbushana na atusaidie kutenda mema, kuwa watii na kuwa watendaji wa Neno.
Posted on: Thu, 04 Jul 2013 20:29:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015