KWA HISANI YA Chumba Cha Siri Baba na mtoto wake walikuwa - TopicsExpress



          

KWA HISANI YA Chumba Cha Siri Baba na mtoto wake walikuwa wakitembea mlimani.Kwa bahati mbaya mtoto akajikwaa na kulia kwa sauti: “AAAhhhhhhhhhhh!!! ” Mtoto alishangazwa kusikia upande wa pili sauti ile ikisikika tena: “AAAhhhhhhhhhhh!!!! Akitaka kufahamu zaidi kwa udadisi kasema kwa sauti: “Wewe ni nani ?” Sauti ikajibu tena: “Wewe ni nani ?” akiwa na hasira kajibu kwa sauti: “Wewe muoga!” upande wa pili sauti ikajibu tena: “Wewe muoga!” Mtoto akamwangalia baba yake na kumuuliza :“Baba mbona huyo mtu mkorofi na ananiigilizia?” Baba akatabasamu na kisha akajibu: “Mwanagu, Hebu sikiliza tena ” kisha baba akapiga kelel akisema: “Nakukubali sana wewe!” Sauti toka pande wa pili ikajibu : “Nakukubali sana wewe” Baba akaita tena kwa sauti na kusema : “Wewe ni bingwa na jasiri sana!”. Sauti ikajibu tena : “Wewe ni bingwa na jasiri sana!”. Yule kijana alishangaa sana ingawa hakuelewa nini kinaendelea. Kisha baba akamfafanulia: “Mwanangu, watu sauti hiyo huiita MWANGWI, kwani huigiza sauti na kuona kama mnabishana na mtu. Lakini MWANGWI huu tunaweza kufananisha na maisha yetu,kwani kila baya au zuri ulisemalo hutokea. Maisha yetu humezwa na matendo yetu tuyafanyayo,. Mfano Kama unahitaji kupendwa na watu wengi hapa duniani, basi pia utatakiwa uandae nafasi ya upendo katika moyo wako pia kwa watu wengine. Kama unatamani uwe na timu ya wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa kujituma,basi wewe uwe wa kwanza kujituma kwa bidii. Kama unapenda kwa na marafiki wenye upendo na kukujali, basi wewe uwe wa kwanza kuwajali na kwapenda Na kanuni hii ukiitumia katika kila kitu maishani mwako, basi utaishi kwa furaha na amani kwani Maisha ni sawa na mwangwi kila utakachokitoa basi tarudishiwa. Kama unataka mpenzi wako asikusaliti basi hakikisha wewe siku zote unakuwa mkweli kwake asubuhi njema wa pendwa
Posted on: Mon, 21 Oct 2013 23:11:45 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015