KWA NINI MUNGU ALUHUSU MAJARIBU.? ndugu zangu majalibu tunaweza - TopicsExpress



          

KWA NINI MUNGU ALUHUSU MAJARIBU.? ndugu zangu majalibu tunaweza kuyafananisha na vishawishi. ni mvuto unaomvuta mtu kutenda,kuwaza,kunena kinyume na mapenzi ya Mungu.majaribu yapo kila mahali, kila siku,kila saa,kila dakika na hata sekunde. jalibu moja linapoondoka lingine linapiga hodi.vyanzo vya majalibu ni kuna majalibu yanayotoka kwa Mungu(ayub:1:12,2:6), shetani(mat:4:3) na ubinadamu wetu (mwili)(yak:1:14-15). SABABU KUU ZA MAJALIBU.zipo sababu kuu mbili za majalibu yote tunayoyapata 1.Ni mtihani au kipimo cha imani yetu. yakob:1:2-3 kwa kadri tunavyopitia kwenye majalibu mbalimbali na tukashinda tunapandishwa ngaza au hatua ya ushindi.Tunapimwa kama kweli tunamwamini sana Mungu na neno lake. ndugu yangu unapopita kwenye changamoto yeyote amini sana neno la mungu ndo maana daudi alisema (moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi. zab:119:11) hivyo kama tutafaulu majalibu ndipo tutakapo pandishwa daraja ya imani. 2.Ni mtihani kwa utii wetu mbele za Mungu.mwa:22:1-19.sisi kama watoto wa Mungu tunapimwa kama kweli tuna utii kwa Baba yetu je kweli tunampenda au tunatimiza tu wajibu, je kweli tu waaminifu kwake. kwa hiyo Mungu hutupima kuona kama tutamtii au tutamtii shetani na Mungu alishaatwambia mtiini Mungu mpingeni shetani naye atawakimbia (yakob:4:7) JINSI MAJALIBU YANAVYOZAA DHAMBI.majalibu si dhambi lakini tunapoyatii majalibu ndipo tunapoanguka dhambini. ndugu zangu kuna majalibu yanayotupata kwa sababu ya kumpa nafasi shetanikatika maisha yetu.na hii inatuletea kuingia dhambini kwa urahisi na Mungu alishasema tusimpe ibilisi nafasi(efeso:4:27).inatupasa kugombana na dhambi mpaka tushinde ndo maana neno la Mungu linasema hamjafanya vita hata kumwaga damu mkishindana na dhambi (ebran:12:4).dhambi ni mbaya sana ilimchinja mwana wa Mungu msalabani.kwa macho ya nyama inaonekana kama tamu sana lakini mwisho wake ni chungu kuliko pilipili na ndani ya dhambi kuna majuto na moto wa milele. Bibilia inasema tukimbie dhambi kama mbele ya uso wa nyoka (joshua bin sira:21:2).dhambi ni kama kidonge cha chororoquine kilichopakwa asali.pia yatupasa tukimbie mazingila ya dhambi ambayo kwayo hufisha roho zetu na baadaye kuanguka dhambini NJIA ZA MAJARIBU.Hizi ni njia ambaza majalibu yanapitia kutupata. 1.kwa kupitia umasikini mith:30:9. pia 2.kwa kupitia mafanikio Tunayopewa na Mungu mith;30:9 Pia 3.kwa kupitia utukufu wa kidunia hes:2;17 na 4.kwa kukata tamaa zab;42:11. MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA MAJALIBU.1.jihadhari sana na kiburi. 2.mtegemee sana Mungu. 3.shangilia ukiwa katika mateso filip:2:13. usionyeshe hali ya huzuni. ndugu yangu ukifahamu uzuri wa majaribu hutaweza kunungunika maana majaribu hututenga kati ya wateule na walioitwa mat:22:14. walioitwa ni wengi sana lakini si wote ni wateule bali wateule ni wale wanaostahimili mateso ufun:17:14 na isay:48:10.na kadili unavyoshinda jaribu moja hadi jingine ndipo nguvu ya ushawishi wa majalibu mengine yanayokunyemeleainapopungua na kuona majaribu mengine kama kitu cha kawaida na hali hiyo ndo kukua kiroho. JINSI YA KUSHINDA MAJARIBU.1.Kusoma sana neno la Mungu na kukaa ndani ya neno la Mungu. yoh:15:7. pia 2.kumkataa shetani na uongo wake. 3.kuikana nafsi yako na kujitwika msalaba wako kila siku Luk;9:23. pia 3.kutambua milango ya majalibu au dhambi hasa zile dhambi zituzingilazo upesi na kukimbia milango yake. 4.kuwa mtu wa sala na maombi ya kila siku. 5.kwa kukubali kupitia mlango mwembamba maana mlango ni mpana uendao upotevuni. 6.jiepushe sana na marafiki wabaya wanaoweza kukuangusha kiroho mda wowote mfano kama umeamua kuacha pombe kama ulikuwa umezoea malafiki ambao ni wanyaji mlikuwa mnakunywa wote anza taratibu kupunguza ukalibukama hawataki kabisa kubadilika. ndugu zangu kukataa au kuacha dhambi si kazi rahisi inahitaji kuchukua maamzi magumu ambayo mda mwingine ulimwengu unaweza usikuelewe. MAOMBI.kama hujampokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako fuatana na mimi kuomba sala hii EE MUNGU BABA MWENYE HURUMA NAKUSHUKURU KWA ZAWADI YA UZIMA NAKUKABIDHI MAISHA YANGU YOTE. NATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOTENDA KWA KUJUA AU KWA KUTOKUJUA NA NINAWASAMEHE WATU WOTE NILIOWAKOSEA NA WALIONIKOSEA NA NINAJISAMEHE KWA KUJIKOSEA MWENYEWE. NAMKATAA SHETANI NA MAMBO YAKE YOTE NA RAHA ZAKE ZOTE NA UONGO WAKE WOTE. BWANA YESU NAKUPOKEA UWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. FUTA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU NA UANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA WA MILELE. ROHO MTAKATIFU NAOMBA UNISAIDIE KATIKA SAFARI YANGU YA WOKOVU.ASANTE YESU KWA KUNIOKOA ASANTE YESU SIFA KWAKO YESU AMINA. Hongera sana kwa kumpokea BWANA YESU Mungu akubaliki,akuinue na akutunze.mungu ni mwema sana yeye ni msaada kwa kila anayekimbilia jina lake mith:18:10.amekuwa msaada na kimbilio langu na atakuwa kimbilio na msaada kwako pia. MUNGU AKUBALIKI. AMINA.
Posted on: Wed, 11 Sep 2013 11:27:52 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015