KWA NINI TUNASHANGAA? Watanzania wenzangu kwa nini - TopicsExpress



          

KWA NINI TUNASHANGAA? Watanzania wenzangu kwa nini tunashangaa:- 1. Obama kufuta ziara ya Arusha wakati kumetokea matukio mawili ya mikusanyiko ya watu kurushiwa mabomu huko huko Arusha bila:- (a) wahusika na ulipuaji huo kukamatwa (tatizo dogo) (b) kuonekana kwa mikakati thabiti ya kuwasaka wahusika (tatizo kubwa) (c) vyombo vya dola kuonekana vimeguswa sana na matukio hayo (tatizo kubwa zaidi) 2. Obama kutoamini vyombo vyetu vya usalama kwa usalama wa watu wake wakiwa hapa wakati vyombo hivyo vinaonekana wazi kutojali matukio makubwa ya kihalifu yanapotokea kama ilivyoelezwa hapo juu. 3. Obama kuweka magari ya misafara yake mafuta aliyokuja nayo wakati hapa gari la Rais wetu liliwahi kuwekewa mafuta ya kuchakachua bila:- (a) wahusika kuchukuliwa hatua (b) mhusika mkuu wa uhalifu huo katika eneo lake la utendaji kuwajibika (c) kutolewa kauli yoyote kali ya kulaani kitendo hicho Kinachotupotezea umaarufu sana sasa hivi Watanzania wenzangu si kutokea kwa matukio makubwa bali ni ile hali ya kutojali kwamba matukio hayo yametokea na kuendelea kuishi kama hakuna kubwa lolote lililotokea! Shambulio la bomu si kitu cha ajabu duniani kwani mashambulio kama hayo yameshajitokeza sana duniani, kukiwepo huko huko Marekani, bali kinachotutia doa Watanzania ni kuona kama matukio hayo ni madogo na ya kupuuzwa! Tuanze sasa kuwa serious na matukio makubwa.
Posted on: Sun, 30 Jun 2013 08:40:49 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015