Kanisani KIDIA, OLD MOSHI, Kilimanjaro-TANZANIA, Africa na Duniani - TopicsExpress



          

Kanisani KIDIA, OLD MOSHI, Kilimanjaro-TANZANIA, Africa na Duniani kote. Nawasalimieni nyote. LEO Nakumbuka siku yangu kuzaliwa 28th August. NINA MSHUKURU MWENYEZI MUNGU KUNIFIKISHA MIAKA 79. Jina la YESU KRISTO LIPEWE SIFA. Amen! Nina kumbuka nikifanya kazi ya Serikali, Ofisi ya Makamu wa pili wa Raisi, 1966-1976,nilikuwa nasali KANISA la AZANIA FRONT,DSM.Nawakumbuka sana Wachungaji :Anael Macha na mke wake Mawere, Loyd Swantz na mke wake Maria Lisa, T.Englund na mke wake,pamoja na Parish worker dada Marta Mandao ambaye tuliwafundisha watoto wa Sunday School katika LUTHER HOUSE: Kila mtoto mwenye birthday yake,tuna mwimbiya "happy birthday".kwangu mwalimu,waliniimbiya,"Happy birhday to you,/ Happy birthday to you,// Happy birthday to YEDEDIA, / Happy birthday to you. 2.GOD BLESS you to day,/GOD BLESS you to day,,// GOD BLESS YEDEDIA,/GOD BLESS you to day." Mwalimu dada Marta alikuja ajiriwa Sauti ya Injili na kuolewa kama Mama Kimaro,na alishafariki,hata Mpendwa Babu Mchungaji Anael Macha,wote wako kwa YESU KRISTO Peponi. Mimi nilistaafishwa 1976 nikaja hapa Moshi pamoja na barua ya kuingiya MAKUMIRA THEOLOGICAL COLLEGE,iliyo wakilshwa huko toka AZANIA FRONT na wachungaji LLoyd Swantz,na MAKUMIRA THEOL.wakajulisha Usharika wangu KIDIA enzi ya Mchungaji Ngowi. Hakuna kilichotekelezwa, na nikaanza kuweka umeme kanisani KIDIA,nyaya,switches,toka WAKRISTO UJERUMANI. Yesu Kristo aliwachagua wanafunzi wake toka nyanja mbali mbali,wengine toka wafua samaki,wengine toka watoza ushuru n.k.; na bado kanisa lina waumini aina zote kipawa cha ROHO MTAKATIFU TOKA MBINGUNI kwa KANISA LA KE YESU KRISTO...
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 06:51:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015