Kethi Kilonzo na Philip Kaloki ambao wametangaza azma ya kuwania - TopicsExpress



          

Kethi Kilonzo na Philip Kaloki ambao wametangaza azma ya kuwania kiti cha usenete katika kaunti ya Makueni wanatazamiwa kubaini hatma yao hii wakati kamati ya kutatua mizozo katika tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC itatngaza uamuzi wake baada ya kuandaa vikao kubaini uhalali wa wawili hao kuwania kiti hicho.Bi Kethi wa chama cha wiper chini ya muungano wa CORD anakabiliwa na tishio la kufungiwa nje kutokana na usajili waka kama mpiga kura na ambao unatailiwa shaka huku Philip Kaloki wa chama cha Narc ambaye analaumiwa kwa kuwasilisha stakbadhi zake kama muda umekamilika baada ya kuhama chama.Iwapo Bi Kethi atapatikana na hatua ya kutumia udanganyifu,chama cha LSK kitaondoa jina lake miongoni mwa orodha ya mawakili na pia kubanduliwa kwenye kinyanganyiro hicho huku Kaloki naye akionja shubiri hiyo kwa kufungiwa nje.
Posted on: Mon, 08 Jul 2013 03:14:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015