Kila jambo huwa na maana yake na kila kitendo humaanisha tofauti - TopicsExpress



          

Kila jambo huwa na maana yake na kila kitendo humaanisha tofauti yake. Leo ni siku nyingine tena watanzania wenzangu nimependa kuzungumza na nanyi kupitia bandiko hili. Watanzania wenzangu napenda tujadili juu ya hili jambo linalotikisa taifa letu kwa sasa tukiachana na yale mengine napenda tuseme tu juu ya MADAWA YA KULEVYA. Kwakweli yamekua gumzo sana kwa mawiki kadhaa yaliyopita kufuatiwa na kukamatwa kwa mwanadada mtanzania kule AFRIKA YA KUSINI akiwa na zaidi ya kilogram 150 za madawa ya kulevya kwakweli hii imekua picha mbaya kwa taifa letu...tukiachana na hilo pia imeripotiwa kuwapo na watanzania ndani ya magereza huko nchini china waliokamatwa kwa madawa haya haya ya kulevya ambayo chanzo chake kinalipotiwa kutokea JULIAS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT (JNIA) Dar es salaam. Hali hii mbaya ndio iliyompelekea hata waziri Dr H.Mwakyembe kuamua kufanyika kwa uchunguzi wa kina na kufikia kuwafuta kazi baadhi ya maofisa katika UWANJA huo wenye jina kubwa kwa taifa kutokana na kupewa jina la baba wa taifa hili MWAKYEMBE Amefanya vile ambavyo amefanya na kutokana na dhamana aliyopewa na serikali yake ya chama cha mapinduzi CCM inayoongozwa na RAIS KIKWETE. Kwa binafsi yangu sijaona kabisa kama kazi aliyoifanya Mh Mwakyembe inaleta majibu ya kukomesha biashara hii ya madawa ya kulevya nchini. Nathubutu kusema kauli hiyo labda kufuatiwa na kauli za viongozi wakuu zaidi ya mtendaji huyu Mh Mwakyembe. Nitawarudisha nyuma kidogo tukumbuke kua RAISI KIKWETE ALISHA WAHI KUSEMA KUA ANAWAFAHAMU WAINGIZAJI WA MADAWA HAYA YA KULEVYA......sasa tangu raisi wetu huyu ambaye ndio mkuu wa serikali alitamka maneno haya kwa watanzania alafu bado akawaacha tu watu hao wakaendelea kuyaingiza kwa kasi kubwa kuendelea kuwaharibu vijina wa kitanzania na kuwaongezea umaskini...hapa napata shaka sana juu ya kiongozi huyu wa nchi...tukiacha kauli hiyo pia ntawakumbusha nyuma zaidi katika bunge la 2005~10 kulikua na dada yetu marehemu AMINA CHIFUPA MPAKANJIA aliyekua mbunge viti maalumu(VIJANA) . Naamini utakua unakumbuka kua alishawahi kusema kuwa anawafahamu wauzaji wa dawa hizo za kulevya tena anaweza akawataja hata kwa majina na yupo tayari kuwataja. .....Lakini baada ya kauli hiyo ambayo ilikua nzito kwa upande wa watuhumiwa ambao marehemu aliwafahamu. Kilichofuata kwa kweli ndicho kilichonifanya kukosa imani na jeshi la polisi pamoja na serikali yangu hii ya CCM.......Na ndio maana hata ikasema kua sina imani na kazi hii nzito inayofanywa na mh MWAKYEMBE ikiwamo na hata kufungwa kwa mtambo wa kukagulia na kutambua madawa hayo na nazidi pia kukosa imani baada ya kauli ya hivi juzi juzi ya Mh WILLIAM LUKUVI waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge alisema kua KAMA TUTATAJA MAJINA YA WAINGIZAJI WA MADAWA YA KULEVYA WABUNGE AMTAPONA HUMU NDANI. Kufuatia na kauli hii ya kiongozi huyu wa nchi mbaye yumo katka ofisi ya WAZIRI MKUU ambapo ndipo kuna kitengo mahususi cha kuthibiti madawa ya kulevya napata uhakika ya kua ni kweli serikali hii ya CCM Inawafahamu vizuri Wauzaji wa madawa haya ya kulevya lakni INASHINDWA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA. Na hapa sasa ndio nakuwa na swali kwaniniiiiii????!!inashindikana najua hayo mambo mengi ya kujiuliza lakini kwa sasa tujiulize hili....MWAKYEMBE WORKDONE IS EQUAL TO NEGATIVE....WAAMBIE VIONGOZI WENZAKO WAJISAFISHE KWANZA.....
Posted on: Sun, 01 Sep 2013 10:26:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015