Kuna day nimeenda kwenye birthday ya Dada mmoja hivi tunaishinae - TopicsExpress



          

Kuna day nimeenda kwenye birthday ya Dada mmoja hivi tunaishinae ktaa imoja..... Ile birthday ilikuwa na raia wengi kias fulani tofauti na birthday zingne.. Nimezama ndani ya hiyo birthday huku nimetupia zangu zile nguo zangu za kipaimara huku chini nimevaa dundo kubwa kichiz. Sasa ikafika muda wa kuzima mishumaa pamoja na kula keki mimi hapo sina time na mtu yoyote yule niko pekeangu pekeangu, bwana we keki ikaanza kuliza huku wakilishana kiundugu undugu, mara aje Baba mara Mama mara bibi mara mjomba,,,,, nikichek hivi keki inakaribia kuisha halafu sisi ambao sio ndugu hatujapata hata kipande nikasema hawa wasitutanie naenda mbio mbio maka pale keki ilipo then naichukua kisha nakimbia.. Nikarudi nyuma kidogo ili nijiandae kwa kutimua mbio kama Usain Bolt vle.. Nikaanza kuhesabu mpaka tatu ili nichomoke then niipitie ile keki nikaanza sasa moj.a......... mbili...... Tatu nikachomoka mbio wewe wacha nile mueleka nikalivaa lile limeza lenye keki kisha nikapiga domo pale kwenye meza meno yote ya mbele pale pale yakatoka.. na keki sikuuambulia zaid ya kuwa mapengo.....
Posted on: Tue, 19 Nov 2013 09:58:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015