Kusafiri kwa Mdaiwa May 29 2011 Anayedaiwa anatakiwa atokane na - TopicsExpress



          

Kusafiri kwa Mdaiwa May 29 2011 Anayedaiwa anatakiwa atokane na deni analodaiwa ili aje kwa Allah akiwa ametakasika na kila jukumu. Likishindikana kwake hilo, asiondoke ila wakimruhusu wanaomdai, na ausie madeni wanayomdai. Haya iwapo deni umefika wakati wake wa kulipwa. Ama ikiwa haujafika wakati wake wa kulipwa, itamjuzia kuondoka bila ruhusa yao kwa sharti ausie wanachomdai. Na haya kwa hali yo yote ni kwa yule aliye nacho cha kulipa; ama asiyekuwa na cha kulipa asiondoke kwenda hija mpaka atokane na kila deni analodaiwa, na Allah ni Aula wa kuukubali udhuru wake. MDAIWA DENI LA RIBA Huyu hali yake ni ngumu mno kuliko aliyetangulia. Ni juu yake kwanza ajitakase na kila muamala wa riba; kwani Allah Mtukufu hawapokelei ila watu wacha-Mungu; na mwenye kuingia katika riba hayumo kabisa katika ucha- Mungu. Inatosha kuwa yeye yumo vitani dhidi ya Allah na Mtume Wake – rehema za Allah na amani zimshukie. MAZINGATIO: � Kukopa kwa ajili ya kuhiji hakuna haja, kwasababu mwenye kuhiji hutakiwa atokane na majukumu yote kabla hajasafiri na miongoni mwa hayo ni madeni. � Wengi kati ya watu huchelewesha hija mpaka wakifikia umri mkubwa huusia wafanyiwe hija iliyowalazimu. Hili ni kinyume na amri ya Allah Mtukufu Mtakasika, kwani wasia hauwi badala ya hija. Mwenye uwezo anawajibika kuharakiza kuhiji mwenyewe; na kuusia ni kuchukua tahadhari tu yasije mauti yakamfika ghafla kabla ya kuhiji. � Kuhiji hakuombewi msaada wa kifedha maana ni fardhi kwa mwenye uwezo wa nafsi na mali. Akifanya hilo kisha baadae akapata uwezo ni bora kwake na salama zaidi arudie hija yake. � Haimlazimu mtoto kuwahijia wazazi wake waliokufa maadamu hawakuusia. Akiwahijia itakuwa ni wema aliowafanyia anaolipwa thawabu na ni utiifu kwa Allah; na wao wanatarajiwa kupata thawabu wakiwa katika watu wa kheri. � Anayesafiri kwenda Maka au Madina au kwengineko inamwajibikia kupunguza sala za rakaa nne ziwe rakaa mbili asiposali nyuma ya imamu mkaazi. Kuisali kila sala kwa wakati wake ni bora, na kuchanganya sala mbili kunajuzu hususan kwa ambaye yumo njiani katika safari. � Hija ni nguzo na fardhi mojawapo ya Uislamu. Uwajibikaji wake na utekelezwaji hautegemei kuoa na kuolewa au ukubwa wa umri, kama wanavyodhani wengi kati ya watu. Bali kuhiji ujanani ni bora zaidi ili mtu aweze kuitekeleza kama ipasavyo kisheria.
Posted on: Fri, 06 Sep 2013 04:28:34 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015