#Kwenye_Michezo_Leo Tanzania yatinga nusu fainali Airtel - TopicsExpress



          

#Kwenye_Michezo_Leo Tanzania yatinga nusu fainali Airtel Rising Stars Lagos, Nigeria. Timu za Tanzania, wavulana na wasichana zimefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars inayoendelea kutimua vumbi jijini Lagos , Nigeria. Timu ya Tanzania ya wasichana leo itacheza na majirani zao Uganda wakati wavulana watakutana na Zambia ambao walitoka sare ya 1-1 katika hatua ya makundi katikati ya wiki. Wasichana wanaingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na wapinzani wao Uganda katika hatua ya makundi Jumatano iliyopita. Kwa upande wa wasichana walifanikiwa kutinga nusu fainali kwa kuifunga D R Congo kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90. Watanzania na mashabiki wa mpira wa miguu barani Afrika wataweza kuona mechi za nusu fainali na fainali ya michuano hii moja kwa moja kupitia Supersport 9. Tamasha la kufunga mashindano ya Afrika ya Airtel Rising Stars leo litapambwa na mwanamuziki wa Nigeria, 2Face Idibia. Michuano hiyo imeshirikisha timu za Kenya, Tanzania, Madagascar, Malawi, Ghana, Zambia, Gabon, DRC, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Uganda, Niger.
Posted on: Sun, 22 Sep 2013 04:59:31 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015