Leo napenda kuchukua fursa hii kuwazindua wazee wenzangu juu ya - TopicsExpress



          

Leo napenda kuchukua fursa hii kuwazindua wazee wenzangu juu ya tatizo tulilonalo kama wazazi, mimi nimo humu kuona mambo yanakwenda sawa na ndiyo maana nimekuwa nikichangia michango na status za vijana na hasa watoto wangu. Kizazi cha millenials kinatofauti mno na changamoto kibao katika malezi, mzazi ukisema ukae mbali na hizi social networks elewa mwanao atajifunza na kufuata ushauri wa watu wengine kupitia mitandao, kwani akili ya mtoto wakati mwengine huwa kama sponge zinavyonyonya maji, Mungu jaalia yawe maji masafi, na je yakiwa machafu? Ukiachia mitandao ikulelee watoto wako, utakuja kuilaumu dunia na maendeleo yake kwa hofu uliyonayo leo ya kuingia kwenye mitandao, kwamba eti ukiingia humu utaonekana mtu mzima ovyo, kicheche, kikaango, baba/mama sukari, ATM, kishubaka, na majina mengi ya ovyo yanayofanana na hayo. Tatizo la kizazi chetu ni la kidunia hakuna hata jamii moja duniani iliyosalimika, labda wale wanaoishi maporini na kukwepa maingiliano na wengine. Ambao wapo misitu ya Tanzania, Angola Congo, nchi za kusini mwa Afrika, Papua New Guinea, China, Indonesia, India, Brazil, Mexico, Columbia, Peru, Tonga, Fiji, Vanuatu, Kiribati na Western Samoa. Sote tuna matatizo yanayofanana ya hiki kizazi kinachoitwa Millenials. Wazazi wanatakiwa waingie kwa wingi kwenye twitter, facebook, tagged, hi5, skype na mitandao mingine ili waweze kuwafuatilia kwa karibu, kuwashauri na kuwaongoza vijana wao, kuna wakati mimi binafsi nawainbox watoto wangu na kuna wakati naweka bayana kila kitu ili iwe fursa kwa vijana wengine kujifunza, na kuwafaa kile ninachowafunza wanangu kupitia mitandao. Ebu tembelea pew/ millenials uone kwanini nimo kwenye hii mitandao, labda baadhi ya wazazi wenzangu watatanabahi na kuzindika na kisha kunielewa, kama mtoto anakuacha mbali mno namna anavyofikiri, kuwaza, kujenga hoja na mitazamo, ambayo anajifunza mitandaoni, itakuwa ngumu mno kwa mzazi kujua namna wanavyofikiri na mitazamo yao, ukifika hapo mzazi utalazimika kuuachia ulimwengu ukulelee wanao kupitia mitandao, weka nia ya kuwafunza wanao na kila mtoto kupitia hii mitandao, asaa ikawa kheri mtoto wako wakaongoka, na wengine wakanufaika na darasa zisizo rasmi, wakaja kuwa vijana wema na wazazi bora kwa kizazi chao na umma kwa ujumla. Wazazi msijitenge na watoto wenu na hii mitandao chonde chonde wazazi, wazazi bado bado tuna jukumu la kuwaongoza watoto wetu hata kama wameoa au kuolewa, mtoto kwa mzazi hakui, na sharti mkumbuke kuwa wazazi tuna dhima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na ipo siku tutaulizwa, kwani kila mmoja wetu ni mchunga, na ipo siku tutaulizwa kwa vile tulivyopewa kuvichunga, ikiwemo, wake, waume, watoto, na wale wali chini yetu kimalezi, kutakuwa hakuna kisingizio cha eti mtoto alikuwa mkubwa akawa na maamuzi yake, ebo! Hata kama ana mambo ya ovyo unashindwa kusema eti mtoto kakua? Hilo kwangu halipo nitaendelea kusema hadi naingia kaburini, ili kesho nisije kuhukumiwa kwa kushindwa kuwaongoza vyema, Mwenyezi Mungu ajaalie kujikumbusha hili na kuwakumbusha wengine inshallah!
Posted on: Mon, 24 Jun 2013 12:23:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015