MAISHA YA NDOA Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba - TopicsExpress



          

MAISHA YA NDOA Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Ukiangalia (Zaburi 45:10-11 anasema, Sikia, binti, utazame (maana yake anazungumza na msichana), utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. maneno haya Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako yana maana kuwa kwenu ndo unatoka maswala ya kurudi kwenu au tatizo kukimbilia kwenu hairuhusiwi ni sawa watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, ambacho ni kitu hakiwezekani. Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya YESU KRISTO. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya YESU KRISTO moyoni mwako ni mume/mke wako. Uamuzi wa kuoa au kuolewa unamtaka mtu aingie katika ndoa asilimia mia moja. Ikiwa hautakuwa tayari kuingia kwenye ndoa kwa asilimia mia moja, tafadhali usiamue kuoa au kuolewa. Utampotezea tu mwenzako muda maana hakuna ndoa isio na matatizo. Lakini pia hakuna tatizo ambalo MUNGU hawezi kulitatua. Lakini, je, uko tayari kushirikiana na MUNGU katika ndoa kwa kiwango cha asilimia ngapi?. Tafakari mpendwa na mshirikishe MUNGU katika ndoa yako na wewe ambao hujaolewa wala kuoa ikabidhi ndoa yako ijayo mikononi mwa MUNGU . JEHOVAH mwenye nguvu akushindie vikwazo vyote na kama hujaokoka kumbuka WOKOVU NI SASA maana hilo ndilo la muhimu kuliko yote ambayo mwanadamu anaweza kuyafanya, Kumpa YESU KRISTO maisha yako ni kupata uzima wa milele maana hakuna uzima wa milele kwingine nje na YESU KRISTO (Yohana 14:6, Matendo 4:12). NI mimi ndugu yako Peter Michael Mabula. Maisha ya ushindi Ministry.
Posted on: Sat, 23 Nov 2013 15:46:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015