MAJANGA YA JANA SI MCHEZO Jana coco beach nimekutana na demu - TopicsExpress



          

MAJANGA YA JANA SI MCHEZO Jana coco beach nimekutana na demu mmoja mkali vibaya mno nikamfwata huku nimeshika chupa ya castle ndani nimeweka maji nazuga nakunywa bia Nikamsalimia nikamuuliza vipi mrembo mbona mtoto mzuri kama wewe umekaa mwenyewe huna kampani?? Akanijibu mimi nimekuja mwenyewe kaka yangu hapa napunga upepo nikiridhika narudi zangu nyumbani Nikamwambia naomba tukae wote tupige japo stori mbili tatu yule mrembo akaniambia poa kaka usijali kaa tu Nimekaa pale na yule mrembo nikamuuliza jina lake akaniambia anaitwa SELINA anakaa KIMARA anafanya kazi ya secretary mimi nikamwambia naitwa JAMAL PEACE nikamdanganya naishi MIKOCHENI nafanya kazi BANDARINI Hapo Mfukoni nilikuwa na ka Elfu tano ka mawazo nikamnunulia Redds ili anione kweli nipo safi tukapiga stori nyingi sana na yule mrembo nikaanza kumtongoza pale akanipa namba yake akaniambia jibu atanipa kwenye simu nilifurahi sana yani kukutana na mrembo mzuri kama yule nikafika home nikaanza kuchati naye yani full kupeana maneno matamu akaniahidi Juma pili lazima aje gheto kunitembelea Leo nimevaa nguo zangu za mgambo nimewahi kariakoo kupambana na machinga jua kali njaa inaniuma balaa sijapewa rushwa yyte na machinga nna hasira balaa Nikasikia kama mtu kanigusa mgongoni kugeuka nyuma namuona yule mrembo ambaye nilimit naye jana coco yupo na rafiki zake wawili akaniuliza we mkaka we si JAMAL PEACE jana tumeonana coco ukaniambia unafanya kazi Bandarini kumbe wewe Mgambo kwanini umenidanganya sasa Dah nimejisikia sana aibu nikabaki nashangaa tu pale hata sielewi nimjibu nini yule mrembo yeye na wenzake wakabaki tu wanacheka huku wananisema na kunitukana mitusi kibao nilivyoona wananijazia watu nimeangalia njia nimetoka nduki nimeacha hadi kirungu changu na kofia watu wote kariakoo wakawa wananishangaa wanajua Mgambo kachanganyikiwa kumbe mwenzao nakimbia majanga Nimeenda kwenye duka moja nimejificha huku nahema balaa nimeaibika sana mrembo alishanielewa kabisa alishanikubalia akaamini mimi nafanya kazi bandanrini na alishaniahidi kabisa leo jumapili anakuja gheto alafu leo kanifumania na nguo zangu za mgambo nagombana na machinga dah bonge la noma yani GONGA LIKE/SHARE/KAMA UMEIPENDA HII STORY
Posted on: Sun, 20 Oct 2013 09:31:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015