MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU ILI KUEPUKA KUSALITIWA. 1.Amini Hawezi - TopicsExpress



          

MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU ILI KUEPUKA KUSALITIWA. 1.Amini Hawezi Kukusaliti Jambo La Kwanza Kabisa Ni Kujenga Imani Kwamba Mpenzi Wako Anakupenda, Anakuheshimu Na Kukuthamini Hivyo Hawezi Kushawishika Kwa Namna Yoyote Ile Kukusaliti. Hii... Itakufanya Kuwa Na Furaha Na Yeye, Pia Utamfanyia Mambo Ya Kumfurahisha. Ukiwa Huna Imani Na Mpenzi Wako, Unaweza Kujikuta Unapunguza Mapenzi Kwake Na Matokeo Yake Ukachochea Yeye Kuanza Kukusaliti. Punguza kumpekua pekua utagundua mengi yatakayokukosesha raha bureee....kama anataka ujue utayajua tu usijipe jakamoyo bure..... 2.Mtosheleze Mpenzi Wako Mchukulie Kama Mtoto. Unapomlisha Unahakikisha Ameshiba Ndiyo Unamuacha. Akitaka Pipi Unamnunulia. Vivyo Hivyo Kwa Mpenzi Wako. Mtoshelezea Katika Kila Nyanja. 3.Muoneshe Upendo Wa Hali Ya Juu, Mpe Heshima Anayostahili Na Pale Mnapokuwa Kwenye Mambo Yetu Yalee, Mpe Hadi Aseme Nimeshiba Mpenzi Wangu. Ukifanya Hivyo Aende Nje Kutafuta Nini? Akienda, Huyo Ana Tamaa Zake Za Kijinga Na Ukibaini Muache Haraka kama hajutii makosa yake. 4.Zungumza Naye Ndiyo, Vunja Ukimya, Zungumza Naye! Si Vibaya Ukawa Unazungumza Na Mpenzi Wako Juu Ya Mambo Yahusuyo Uhusiano Wenu. Muulize Ni Mambo Gani Ukimfanyia Anasikia Furaha, Akikuambia Na Mambo Hayo Yakawa Ndani Ya Uwezo Wako, Jitahidi Kumtimizia. 5.Muulize, Anachukizwa Na Mambo Gani, Akikuambia Basi Jiepushe Nayo. Hata Asipokuambia, Ukimchunguza Utayabaini Tu. Hayo Ni Baadhi Tu Ya Mambo Ambayo Ukiyazingatia Yanaweza Kukusaidia Katika Kumfunga ‘Spidi Gavana’ Kimtindo Mpenzi Wako Ili Asikusaliti. Kama Itatokea Akakusaliti Licha Ya Kumfanyia Yote Hayo, Huyo Siyo Mtu Wa Kuendelea Kuwa Naye........
Posted on: Mon, 16 Sep 2013 18:52:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015