MATUMIZI YA TEKINOLOJIA YA VINASABA VYA BINADAMU -TANZANIA 1.0 - TopicsExpress



          

MATUMIZI YA TEKINOLOJIA YA VINASABA VYA BINADAMU -TANZANIA 1.0 UTANGULIZI Tekinolojia ya vinasaba vya binadamu inafanya kazi kwa kusimamiwa na sheria namba 8, sura ya 73, ya mwaka 2009. Sheria hiyo inaitwa The Human DNA Regulation Act, [Cap 73, 2009] ambayo inasimamia na kudhibiti matumizi ya tekinolojia ya vinasaba vya binadamu. Mkemia Mkuu wa Serikali ndiye msimamizi wa utekelezaji wa sheria hii. Taarifa fupi ya umuhimu wa tekinolojia ya vinasaba vya binadamu inavyosaidia katika matukio mbalimbali nchini Tanzania . 2.0 UCHUNGUZI WA VINASABA Uchunguzi unaohusisha tekinolojia ya vinasaba, unahusisha vielelezo vinavyotokana au kupatikana katika mashauri au matukio yafuatayo: a. Mauaji b. Majanga c. Ubakaji d. Wizi /Wizi wa kutumia silaha. e. Uhamiaji f. Uhalali wa mzazi kwa mtoto g. Utambuzi wa binadamu h. Utambuzi wa Jinsi Tawala 3.0 MIFANO HALISI YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA VINASABA VYA BINADAMU Baadhi ya matukio au mashauri yaliyohusisha matumizi ya Tekinolojia ya vinasaba vya binadamu yamechanganuliwa kama ifuatavyo: s/n Aina ya tukio TUKIO Matumizi ya Tekinolojia ya vinasaba vya binadmu Maoni/hoja 3.1 Mauaji ya Albino na Vikongwe • SHINYANGA-3(2009) • KAGERA-3(2009) • SUMBAWANGA-2(2013) Kesi mbili(2) tayari zilishatolewa hukumu kutegemea na matokeo ya uchunguzi wa DNA 3.2 Majanga • Milipuko-Mbagala(2010) DAR • Moto: Shule ya Idodi-IRINGA • Kuanguka kwa Jengo- Mtaa wa Kisutu.(2013). • Ajali ya Ndege Comoro.(2010)-Mafia/Dar Askari 6 walitambuliwa na mabaki ya marehemu kuchukuliwa na ndugu wa Marehemu kwa ajili ya kuzikwa. Mabaki ya Marehemu , wanafunzi 12 walitambuliwa na makaburi kutambuliwa. Mabaki ya sehemu ya miili ya marehemu 23 yaliweza kutambuliwa Mabaki ya miili ya marehemu 25 iliweza kutambuliwa na ndugu kuchukua kwa ajili ya kuzika 3.3 Ubakaji/Mimba za utotoni. Mkoa wa MBEYA –(2013) Uchunguzi umesaidia upelelezi na Mahakama Katika kesi za kuwapa mimba mwanafunzi wa shule/wasichana chini ya umri 18. 3.4 Uhamiaji • Mbeya • Ngara-Kagera: Mwanachi kutoka nchi nya nje kudai kuwa na uhusiano na na ndugu ntanzania Tekinolojia ya vinasaba ilitumika na kudhihirisha kuwa hawana uhusiano na wananchi waliowataja nchini Tanzania 3.5 Wizi/wizi wa kutumia silaha • Wizi wa benki NMB(2006) • Wizi wa benki ya West Bureau De Change Uchunguzi umesaidia upelelezi na Mahakama katika kubaini wa husika 3.6 Human trafficking( biashara haramu ya binadamu • Miili ya binadamu iliyopatikana: Morogoro • Dodoma • Kibaha Utambuzi wa binadamu kwa miili iliyopatokana 3.7 Uhalali wa mzazi kwa mtoto Katika kipindi cha Mwaka 2010-2012: 51.68%-Kuhusisha(watoto ni wao) 48.32%-Kutohusisha(watoto sio wao) 3.8 Utambuzi wa Jinsi tawala Katika kipindi cha Mwaka 2010-2012 2.49%-Utambuzi wa jinsi tawala 4.0 MATARAJIO YA BAADAE Mkemia Mkuu wa Serikali kupitia wizara mama ya Afya na Ustawi wa Jamii inamatarajio yafuatayo: i. Kuhusisha Nyanja za tafiti ii. Kuwepo kwa database ya vinasaba vya binadamu iii. Usajili na ukaguzi wa taasisi zinahusisha matumizi ya tekinolojia ya vinasaba vya binadamu
Posted on: Mon, 22 Jul 2013 06:56:27 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015