MAWASILIANO BINAFSI SAA ZA KAZI SHERIA ITUNGWE ITAKAYOKATAZA - TopicsExpress



          

MAWASILIANO BINAFSI SAA ZA KAZI SHERIA ITUNGWE ITAKAYOKATAZA WATUMISHI KUINGIA NA SIMU OFISINI.-MOROGORO Afisa kazi mfawidhi wilaya ya Morogoro Mh Swai simbo, ameitaka serikali kutunga sheria madhubuti itakayozuia wafanyakazi wa serikali kutumia simu binafsi pindi wanapokuwa kazini. Akizungumza na Pambazuko Fm Ofisini kwake , Mh Simbo amesema kuwa hairuhusiwi kufanya mawasiliano binafsi saa za kazi,hivyo ni vyema serikali ikadhibiti vitendo hivi kwa kutunga sheria itakayokataza watumishi wa umma kuingia na simu binafsi kazini. Akiendelea kuelezea kero hiyo ya watumishi wa umma amesema kuwa, maongezi ya nje ya ofisi wakati wa kazi ni sawa na matumizi mabaya ya madaraka. Sanjari na hayo amesema wananchi hawatendewi haki na watumishi wa serikali, kutokana na matumizi makubwa ya simu binafsi hivyo kupelekea kurudisha nyuma jitihada za raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Jakaya mrisho kikwete za kuleta mandeleo ya haraka kwa Taifa .
Posted on: Thu, 14 Nov 2013 08:11:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015