MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa(CCM) Lita Kabati ametoa - TopicsExpress



          

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa(CCM) Lita Kabati ametoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 6.3 kwa shule za msingi zilizoko mkoani hapa. Kabati akizungumza wakati akikabidhiwa madawati hayo kwa ufadhili wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania mwishoni mwa wiki, alisema shule nyingi mkoani hapa zina upungufu mkubwa wa madawati hivyo ni jukumu la kiongozi kuweza kusaidia kuondokana na hali hii na kuwashukuru bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania. “Nimefanya ziara katika shule za msingi nyingi za mkoani kwangu kuna matatizo mengi kama ukosefu wa madawati na vitabu ndipo nikawaomba wenzetu wa bodi ya michezo kubahatisha wanisaidie madawati kwa shule hizi hakika ninawashukuru sana hakika haitamaliza tatizo lakini itasaidia kupunguza japo kwa uchache” alisema Kabati Alisema kuwa elimu bora kwa wanafunzi wa shule za msingi unaendana na vifaa wanavyotumia katika kupata elimu ya msingi ikiwemo kakaa katika madawati bora kunachangia maendeleo ya taifa letu katika kukuza elimu.
Posted on: Wed, 11 Sep 2013 02:56:56 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015