MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA KUWEKWA NDANI YA MFUKO WA SAFETI BAADA - TopicsExpress



          

MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA KUWEKWA NDANI YA MFUKO WA SAFETI BAADA YA KUFUNGWA JIWE ZITO SHINGONI Na, Ngaiwona Nkondora. Songea Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha myonga Peramiho songea vijijini mkoani Ruvuma amekutwa akielea kwenye bwawa la samaki akiwa amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Geoger Chiposi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana saa nane mchana katika bwawa la samaki linalomilikiwa na seminari kuu ya Peramiho kanisa katoriki jimbo kuu la songea. Chiposi alisema kuwa wasamalia wema waliokuwa wakipita karibu na bwawa hilo waliona mwili wa marehemu E vanjelister Lusinga(53) ukiwa unaelea ndani ya bwawa hilo. Alisema kuwa mwili huo ulikuwa umewekwa ndani ya mfuko wa safety huku shingoni akiwa amefungwa jiwe kubwa kwa kutumia kamba ya katani na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu aliuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani. Aildha polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo la kikatili na hakuna mtu anaye shikiliwa kwa ajili ya mahojiano.
Posted on: Fri, 11 Oct 2013 20:48:26 +0000

Trending Topics



/b>
A origem do Sábado está diretamente relacionada à obra de Deus
****AS LOW AS 2,167 MONTHLY **** Second City Drive

Recently Viewed Topics




© 2015