MWANASHERIA WA KENYA AISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU - TopicsExpress



          

MWANASHERIA WA KENYA AISHITAKI ISRAEL KWA KIFO CHA YESU KRISTO. Mwanasheria mmoja nchini Kenya aitwaye Dola Indidis, amefungua mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya The Hague nchini Uholanzi, akizishtaki Serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu Kristo. Mwanasheria huyo, amesema kuwa lazima Serikali za Mataifa hayo ziwajibike kwa kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya Kikristo ( Yesu Kristo ) aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia yoyote ya kustahili adhabu hiyo . Serikali ya Italia inashtakiwa kwa kula njama (conspiracy) za kumuua Yesu, huku Serikali ya Israel ikishtakiwa kwa uzembe wa kushindwa kumlinda Bwana Yesu (Negligence) hali iliyotoa mwanya wa Kristo kuuawa kwa kikatili. Badhi ya watu walioorodheshwa katika hati ya mashtaka ni pamoja na Mfalme wa iliyokuwa himaya ya Roma (Roman Empire), Tiberio, Gavana wa Uyahudi wakati huo Pontio Pilato, na Mfalme Herode. Pia wapo viongozi wa kiyahudi wakiwemo mafarisayo, masadukayo, waandishi na wanasheria ambao wanatajwa kuwa kwa pamoja walikula njama ya kumuua Bwana Yesu. Wakili huyo ambaye amejizolea umaarufu sana kimataifa, amesema anafikiria pia kumuunganisha Yuda Iskariyote katika kesi hiyo kwa kitendo chake cha kumsaliti Bwana Yesu. NINI MAONI YAKO JUU YA KESI HII? JE MWANASHERIA HUYU WA KENYA (DOLA INDIDIS) ANA HOJA ZENYE MANTIKI AU ANATAFUTA TU UMAARUFU?
Posted on: Sat, 10 Aug 2013 11:11:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015