Maalim Seif Shariff Hamad Ndiye Mtu Pekee Anayeweza Kuleta Miujiza - TopicsExpress



          

Maalim Seif Shariff Hamad Ndiye Mtu Pekee Anayeweza Kuleta Miujiza ya Uchumi Zanzibar Hivi karibuni katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad ametangaza nia yake ya kugombea tena kiti cha urais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, kauli yake hiyo kwenye vyombo vya habari imepokewa kwa hasira na chama cha mapinduzi (CCM)..!! Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Zanzibar (UVCCM) wamekuwa mstari wa mbele katika kumshutumu kulingana na msimamo wake huo, lakini tujiulize ni kwanini UVCCM ndiyo wajitokeze kumpinga Maalim Seif kuhusu uamuzi wake huo na siyo umoja wa vijana wa CUF..!? UVCCM wanatia aibu na wanadhihirisha ni namna gani wanavyomuogopa Maalim Seif, na ndiyo maana hawataki kabisa kushindana naye.!! Ikumbukwe kwamba Maalim Seif Shariff Hamad amegombea kiti cha urais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa vipindi vinne mfululizo (1995, 2000, 2005, 2010) na hajawahi kushindwa na mgombea yeyote wa CCM katika nafasi hiyo kwa vipindi vyote vinne..!! Hii ndiyo sababu kubwa inayowapa kiwewe UVCCM kwa vile wanafahamu fika kwamba hawana mgombea mwenye sifa za kuweza kumshinda Maalim Seif (Simba wa Nyika). Natafakari ni nani anaweza kumsumbua Maalim seif ndani ya CCM simuoni, naona wote ni wachovu ambao hata hawana mawazo binafsi bali ni watu wakutegemea sera za CCM makao makuu ambao nao hawana lolote zaidi ya sera za ufisadi na kuchakachua matokeo..!! Maalim Seif ni mchumi mzuri sana, na ni mchapakazi na mbunifu wa hali ya juu; kwa wale wakazi wa Zanzibar wanamkumbuka utendaji wake wa kazi na ubunifu alipokuwa waziri kiongozi chini ya utawala wa Mzee Abdul Wakil..!! Maalim Seif alikuwa anatisha na alikuwa anaogopewa sana na wafanyikazi wa Serikali kwa kuwa na misimamo inayosimamia maslahi ya umma wa Zanzibar; Maalim Seif ni miongoni wa viongozi wachache sana wa Zanzibar ambao ni waadilifu na wazalendo, hata ukichunguza kwa undani utakuta kwamba Maalim Seif waligombana na Mwalimu Nyerere na kufukuzwa kwenye chama cha CCM baada ya kuonekana kwamba ameusimamia Uzanzibar zaidi kuliko kitu kingine chochote kile! Jambo ambalo halikumfurahisha Mwalimu Nyerere ambaye baada ya hapo alianza kumchukia Maalim Seif kwa hulka yake hiyo ya kujiona, kujisikia na kuitetea Zanzibar na maslahi yake yote.! Baada ya hapo Mwalimu Nyerere akaanzisha misamiati ya kusema kwamba kuna “Uzanzibar” na “Uzanzibara”; akiwa na maana kwamba Uzanzibar ni wale wenye asili ya Kiarabu (Waarabu au wale wote wenye damu ya Kiarabu); na Uzanzibara akiwa na maana kwamba ni watu ambao ni Wabantu (Watu weusi wasiokuwa na asili yoyote na Uarabu). Hapa ndipo Wanzanzibar walipoanza kugawanywa kama taifa na wakagawanyika..!! Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana la kisiasa kwa nchi ya Zanzibar kukubali Mwalimu Nyerere awagawe makundi mawili wakati wao ni watu wa taifa moja..!! Wazanzibar walipokubaliana na mawazo ya Nyerere kwamba kuna Wazanzibar na Wazanzibara, basi ndiyo wakawa wamegawanywa makundi mawili kifikra na kujikuta kwamba Wazanzibara wanabakia CCM na Wazanzibar wanahamia CUF..!! Wagawanye ili uweze kuwatawala (Divide and Rule), hiyo ndiyo silaha iliyotumika kuwagawa wananchi wa Zanzibar na wakajikuta wamekuwa wadhaifu na mambo yao na matatizo yao wanajadiliwa Dodoma na siyo Unguja wala Pemba..!! Hili liliwezekana kwa vile Wazanzibara wameungana Watanzania Bara (Watanganyika) na kuwa na nguvu zaidi kuliko Wazanzibar na hivyo kujikuta kwamba umoja wa kitaifa wa Zanzibar ukawa haupo kwa miaka mingi..!! Zanzibar likawa ni taifa lakini halijitambui kama taifa kwa vile nusu ya wananchi wake wakawa wameegemea zaidi bara kiroho na kifikra licha ya kwamba kimwili wanakaa na kuishi visiwani Zanzibar..!!! Ni umakini na umahiri wa kufikiri na kuona mbali wa Maalim Seif Shariff Hamad ndiyo ambao umeiwezesha nchi ya Zanzibar kuunganisha raia wake ambao walitenganishwa na Mwalimu Nyerere kwa maslahi ya kisiasa, na sasa hivi taifa la Zanzibar limerudi tena na kuwa na umoja wa kitaifa kama enzi zile za utawala wa Mzee Abeid Aman Karume..!! Kwa dhambi hii ya kuligawa taifa la Zanzibar, kama kuna hukumu za kisiasa mbele ya mungu, basi kwa dhambi hii Nyerere hataikwepa itabidi lazima ahukumiwe na mungu kwa kosa la kuwagawa Wazanzibar wakashindwa kabisa kuungana na kutetea maslahi ya taifa lao kwa miaka mingi sasa..!! Zanzibar imekuwa ikiongozwa na viongozi ambao wanachaguliwa Dodoma, na wanachaguliwa si kwa makusudi ya kuwasaidia Wazanzibar, hapana, wanachaguliwa kwa maslahi ya kulinda maslahi ya Watanzania.!! Sasa utalindaje maslahi ya Tanzania kwanza kabla hujalinda maslahi ya Zanzibar..!!?? Na hii ndiyo sababu kubwa ambayo imesababisha wananchi wa Zanzibar licha ya kuwa wachache na rasimali nyingi lakini wanaishi maisha magumu kupita kiasi.! Wazanzibar wamebakia watu wa kunywa UJI (Mdabwado) mchana na jioni tangu wamekubaliana na mgawanyo wa Nyerere wa uZanzibara na uZanzibar..!! CCM imeshindwa kuweka mikakati endelevu ya kuwatoa wananchi wa Zanzibar kwenye bahari ya umasikini, licha ya kwamba visiwa hivyo vina watu wa chache na rasimali nyingi ikiwa ni pamoja na mafuta na gesi..!! Watu wengi wahamjui Maalim Seif vizuri na ndiyo maana wanahamaki na kumponda wanaposikia akidai kwamba bado anania na ataendelea kugombea urais wa Zanzibar; ikumbukwe ile program ambayo ilimpa Marehemu Edward Moringe Sokoine ya kuwakamata wahujumu uchumi ilibuniwa na Marehemu Sokoine akishirikiana Maalim Seif, na ni Maalim Seif ndiye aliyekuwa anawasha moto kule visiwani Zanzibar hadi wahujumu uchumi wa kisiwa hicho wakahamia baharini na mashua zao, na wengine walikimbilia visiwa vya Comoro na huko Mombasa – Kenya..!! Pia Maalim Seif ana ushawishi na mvuto mkubwa kwa Diaspora ya kiZanzibar inayoishi nchi mbalimbali duniani, hasa nchi za Kiarabu na hivyo kama atakuwa Rais wa Zanzibar ana nafasi nzuri na kubwa ya kushawishi uwekezaji wa mabillioni mengi ya dollar za Kimarekani katika visiwa hivyo na kubadilisha uchumi wa visiwa hivyo na maisha ya wananchi wake kwa ujumla, tena kwa kipindi kifupi sana kijacho..!! Pia Maalim Seif anakubalika sana na viongozi wengi wa nchi za Kiarabu ambazo hivi sasa ni nchi tajiri na zimekuwa zikiwekeza kwenye nchi mbalimbali duniani kama ambavyo nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (The Tigers) wanavyofanya..!! Tukumbuke na tuelewe kwamba uwekezaji kwenye nchi za bara la Afrika hautegemeani na siasa za nchi, bali hutegemea sana nani yupo madarakani? Na hii inatokana na nchi za Kiafrika kutokuwa na siasa za kudumu, siasa zetu zimekuwa za vipindi vifupi vifupi na hivyo wawekezaji wanakuwa waoga kuwekeza tu kama ambavyo wanafanya kwenye mabara mengine. Sasa kulingana kigezo hicho muhimu kwa nchi yoyote ile inayotaka maendeleo, Maalim Seif Shariff Hamad ana Mvuto huo kwa nchi wawekezaji, hasa zile nchi za Kiarabu ambazo sasa hivi zimegeuka kuwa nchi wawekezaji wakubwa duniani kote. Kulingana ukweli huo hasa nikizingatia hekima, busara, uadilifu na weledi wa Maalim Seif Shariff Hamad ndiyo maana nasema kwamba ndiye kiongozi pekee visiwani Zanzibar anayeweza kurekebisha maovu yote yalitengenezwa na Serikali ya CCM na kuujenga uchumi wa visiwa hivyo kwa muda mfupi na kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa, kiuchumi na maendeleo kwa ujumla..!! Napenda kuwatahadharisha Wazanzibar wote kwamba ni Maalim Seif Shariff Hamad ndiye mtu kiongozi pekee anayeweza kuwaondoa Wazanzibar kwenye janga la umasikini wa kunywa UJI (Mdabwado) mchana na jioni..!! Wengi wanaompinga Maalim Seif ni wale ambao bado fikra zao zimejaa ile kasumba ya Nyerere ya uZanzibara..!!! Achaneni na fikra za falsafa za Nyerere, Nyerere alishindwa maisha kama Mwanasiasa, hivyo ukikuta mtu anamsifia au anamnuu jua kwamba huyo siyo mtu makini na ni mzembe wa kuchambua na kutafakari historia ya kweli ya nchi hii…!!! UVCCM wanamuhofia sana Maalm Seif kwa vile wanajua kwamba hashindwi (Hapigiki) hata siku moja, hivyo wana hofu kubwa kama ikiundwa tume huru itakuwaje? Wanahofu kwamba Maalim Seif atashinda uchaguzi mkuu na hivyo anaweza kuhoji uhalali wa tume ya uchaguzi Zanzibar ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kumnyang’anya ushindi mara nne mfulululizo, na ubalozi wa Marekani na jumuiya ya Ulaya wakiunga mkono kwa kisingizio cha Ugaidi..!!!! Ugaidi wa kutengenezwa na Serikali ya CCM ilishirikiana na vyombo vyake vya ulinzi na usalama..!!! Dr. Noordin Jella noordinjella.livejournal
Posted on: Tue, 05 Nov 2013 14:15:28 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015