Mahakama ya kimataifa ya ICC imeiruhusu Kenya kuwasilisha maelezo - TopicsExpress



          

Mahakama ya kimataifa ya ICC imeiruhusu Kenya kuwasilisha maelezo yake kuhusu hatua yake ya kutaka kujiondoa kwenye mkataba unaobuni mahakama ya ICC. Mahakama hiyo ambayo inasikiza kesi ya naibu rais William Ruto na mwanahabariJoshua Sang imemtakamwanasheriamkuu wa Kenya Githu Muigai kuwasilisha maelezo hayo mahakamani kufikia tarehe 16 mwezi huu. Washirika wengine ambao wanataka kujihusisha na kesi hiyo pia wamepewa nafasi ya kuwasilisha maelezo yao huku mahakama hiyo ikijaribu kuangazia hatua ya mabunge ya Kenya kupitisha hoja ya kujiondoa. Huku hayo yakijiri waziri wa maswala ya kigeniamina Mohamed amesisitiza kuwa Kenya haijaomba muungano wa AU kuandaa mkutano maalum siku ya jumamosi kujadili hatua ya kujiondoa kwa pamoja katika mkataba huo wa Roma. Amina ametupilia mbali madai kuwa mkutano huo kuandaliwa nchini Ethiopia unalenga kujadili hatua hiyo
Posted on: Wed, 09 Oct 2013 14:59:54 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015