Maisha bana, upo ndani ya dala dala na limejaa saaaana!! - TopicsExpress



          

Maisha bana, upo ndani ya dala dala na limejaa saaaana!! umeshikilia bomba tu na ndani mmesongamana sana, huku umeshikilia bahasha yako ya kaki kubwa unawahi ofisini/chuoni/kutafta kazi!!ama upo ktk mishe zako!! Mnaposimama kwenye mataa/ kwenye foleni pembeni unaona kuna gari nzuri sana imesimama nayo, na haina TINTED so unashuhudia kila kitu ndani!! Unamuona Binti mdogo tu au kijana mdogo tu wa kiume yupo ndani ya gari zuri saaana mbele lina ka-screen kadogo/aaaf pale juu ana simu kubwa kubwa kama nne hivi, mara ashike hii mara ashike ile, apo ww unashuhudia tu ukiwa umekamatia bomba lako ndani ya dala dala!! JASHO LIKIKUTOKA AAAAF KICHWANI UNA MAWAZO HINHA!! Yule mtu anakula KIPUPWE tu ndani ya ndinga lake hana habari!! aaaf kama unaona anafanya makusudi vile mara aminye minye ka-tv kake,mara aongeze/apunguze sauti/ mara katoa box la juice kanywa!! yani kama anakuringishia hivi!!! Hhahahahahahahahah!! Katika hali hii ni sentesi zipi zitakuwa zikikujia ktk kichwa chako? Basi na hayo ndiyo jinsi maisha yalivyo!! Mwenye AC ofisini usimcheke mwenye feni tuna toauti/ Na mwenye feni usimcheke anayejipepea na gazeti/ Ndiyo tafsiri ya maisha vijana Mungu alaumiwe kwa lipi?/ Maana wa mwisho atakuwa wa kwanza ila wa kwanza ataenda kati/ MUWE NA SIKU NJEMA MARAFIKI WA R.O.M.A!!
Posted on: Tue, 22 Oct 2013 07:44:23 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015