Majeshi ya Kenya na Sierra Leone ambayo yamekuwa yakipiga doria - TopicsExpress



          

Majeshi ya Kenya na Sierra Leone ambayo yamekuwa yakipiga doria kwenye bandari ya Kismayo nchini Somalia chini ya mwamvuli wa umoja wa Afrika - AMISOM yataondoka katika eneo hilo hivi karibuni. Hii ni baada ya serikali ya Somalia kulalamika kuwa wanajeshi wa Kenya wamekuwa wakiwachagua viongozi ambao wanafaa kuliongoza eneo hilo bila idhini ya serikali kuu mjini Mogadishu. Uamuzi huu ulichukuliwa mjini Kampala kwenye kikao cha marais ambao nchi zao zinachangia wanajeshi nchini Somalia, kilichofanyika jana jioni. Je, Serikali ya Somalia itaweza kudhibiti usalama Kismayo bila ya majeshi ya Kenya?
Posted on: Mon, 05 Aug 2013 09:59:32 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015