Majeshi ya Rwanda, RPF yamevuka mpaka na kuingia Republique - TopicsExpress



          

Majeshi ya Rwanda, RPF yamevuka mpaka na kuingia Republique Democratique du Congo (DRC) yakiyapiga majeshi ya DRC, hata hivyo yamezuiliwa kwa nguvu za majeshi imara ya kulinda amani yaliyo chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa (United Nations) yajulikanayo kama MONUSCO (United Nations Organisation Stabilisation Mission in the Congo). Majeshi ya MONUSCO kwa kifupi ni jeshi la Tanzania. Hii maana yake nini? Ni kwamba: Jeshi la Rwanda, RPF linapigana sasa na jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ uso kwa uso! Je huu si mtego wa uchokozi wa Rwanda kwa Tanzania kutupima nguvu zetu? Ama huu bado ni mwendelezo wa mission ya Rwanda kuhakikisha DRC ya mashariki haitawaliki ili waendelee kuvuna raslimali za kule?
Posted on: Thu, 29 Aug 2013 16:54:50 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015