Majibu ya Tundu Lissu hapo chini dhidi ya tuhuma za Rais Kikwete - TopicsExpress



          

Majibu ya Tundu Lissu hapo chini dhidi ya tuhuma za Rais Kikwete kwake yananikumbusha lile sakata la fitna dhidi ya wabunge waliokuwa wamejiandaa kupambana na kashfa ya manunuzi ya mafuta ambapo yeye alikuwa mstari wa mbele kuwatuhumu wabunge kuwahusisha na ufisadi. Alipoitwa katika tume ya bunge kutoa ushahidi wake akaishia kudai yeye aliitwa na Waziri na Katibu wa Wizara ya Madini na Nishati na kuambiwa akaseme hayo hivyo yeye siyo wa kulaumiwa kana kwamba yeye hana jukumu la kuhakiki anachoambiwa kabla ya kukitumia katika mradi wake wa fitna na uadui dhidi ya wengine. Utetezi wa sasa ni huu “Sasa hapo uongo na uzandiki wangu ni nini, labda hao wawakilishi wa TEC na CCT walisema uongo, hata wawakilishi wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania nao waliieleza kamati kuwa majina waliyoyapendekeza, sio ambayo Rais aliteua” alisema Lissu.
Posted on: Mon, 07 Oct 2013 06:52:53 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015