Mashirika makubwa ya habari ulimwenguni, yapo kwenye vita nzito ya - TopicsExpress



          

Mashirika makubwa ya habari ulimwenguni, yapo kwenye vita nzito ya kugombea hakimiliki ya mazishi ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,Nelson Rolinhlala Mandela ‘Madiba’. Shirika la Habari la Afrika Kusini (SABC),kwa sasa lipo kwenye mzozo na lile la Uingereza (BBC),mvutano uliopo unahusu chombo chenye haki ya kuwa cha kwanza kutangaza taarifa zote zitakazohusu mazishi ya Mzee Madiba. Awali SABC ndicho chombo kilichotajwa kama cha kwanza kupewa hakimiliki ya matangazo yote ya mazishi ya Madiba lakini taarifa mpya ni kwamba mjukuu wa Mandela, Mandla Mandela,37, anadaiwa kuvutiwa na dau nono la BBC,hivyo kuliuzia haki zote shirika hilo la Uingereza. Inadaiwa kuwa BBC limempa Mandla, randi 3,000,000 (zaidi ya shilingi milioni 615), hivyo kulinyima haki SABC ambalo awali lilikuwa limetoa randi 2,000,000(zaidi ya shilingi milioni 326).
Posted on: Tue, 02 Jul 2013 09:21:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015