Mashirika ya kijamii na makundi ya kutetea haki za binaadamu bila - TopicsExpress



          

Mashirika ya kijamii na makundi ya kutetea haki za binaadamu bila shaka yameleta mchango mkubwa katika kupatikana kwa katiba mpya nchini Kenya na kuhakikisha kuwepo kwa utawala wa sheria. Yamechangia sana pia katika miaka iliyopita kuimarisha utawala bora katika kuhakikisha kuna uwazi na uwajibikaji serikalini. Lakini sasa kuna hali iliyojitokeza inayoonyesha juhudi na harakati za makundi haya zinapwaya. Katika mahojiano na idhaa hii, mwanaharakati wa kutetea haki za binaadamu nchini Kenya, Al Amin Kimathi, anasema makundi haya yameathiriwa na siasa na baadhi yao yanatoa ushauri wa kitaalamu kwa serikali na kulipwa fedha kwa huduma zao. Baadhi ya wanachama wamepata kazi serikalini hivyo kuifanya vigumu kwa mashirika hayo kuikosoa serikali wakati inapohitajika. Je, nini mustakabali wa harakati za mashirika haya nchini Kenya?
Posted on: Mon, 30 Sep 2013 14:27:41 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015