Mfalme mmoja aliamrisha jambo,moja wa waziri wake - TopicsExpress



          

Mfalme mmoja aliamrisha jambo,moja wa waziri wake akamkosea,Akaamua amuadhibu waziri huyo kwa njia ya pekee,Nayo ni kuwakusanya mbwa wake wote wakali,kuwafungia na kuwalaza na njaa,kisha waziri aingizwe katika mbwa hao,Waziri akamlalamikia mfalme wangu mbona wataka kuniadhibu na mimi nimekuhudumikia miaka 10?Mfalme akasema nitakuadhibu hivyohivyo!Waziri akasema basi naomba siku kumi tu kisha ndio uniadhibu!Mfalme akamwambia nimekupa siku 10 tu!Waziri akaenda wanapofugiwa mbwa wake,akamuomba mlinzi afanye kazi ndani yake siku 10 ya kulisha mbwa,kuwanywisha na kuwahudumikia,Mlinzi akamuuliza kisha wafaidika na nini? Waziri akajibu nitakwambia baadae!Siku kumi zilipofika akaitisha mbwa wote wakali na yule waziri aletwe,Mara mbwa wote wamkimbilia waziri na kumramba miguu na wala hawamfanyi lolote!Mfalme akashangaa,akasema kuna nini jamani?Waziri akamjibu; hawa ni mbwa nimewahudumikia siku 10 tu wamekumbuka fadhila yangu,ama wewe binadamu nimekuhudumikia miaka 10 umesahau fadhila zote!
Posted on: Thu, 20 Jun 2013 05:17:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015