Mheshimiwa Cheyo amzawadia Rais Kikwete ng’ombe Mbunge wa - TopicsExpress



          

Mheshimiwa Cheyo amzawadia Rais Kikwete ng’ombe Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki, Mheshimiwa John Momose Cheyo wa Chama cha UDP na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho ametoa zawadi maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Mheshimiwa Cheyo ametoa zawadi hiyo kwa Mheshimiwa Rais katika sherehe maalum iliyofanyika asubuhi ya jana, Alhamisi, Novemba 28, 2013, mjini Bariadi Mkoani Simiyu wakati wa halfa ya kutawazwa kwa Rais Kikwete kuwa Mtemi wa Kabila la Kisukuma. Hafla hiyo ya kutawazwa kwa Rais Kikwete ndilo lilikuwa tukio la kwanza katika siku ya tatu ya ziara ya siku tano ya Rais Kikwete katika Mkoa wa Simiyu, shughuli ambayo imehudhuriwa na mamia kwa mamia ya wakazi wa Bariadi. Wakati wa hafla hiyo, ilitangazwa kuwa Mheshimiwa Cheyo, kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Itilima, alikuwa amemzawadia Rais Kikwete ng’ombe mitamba miwili kutoka shamba la mifugo la Mabuki. Mheshimiwa Cheyo mwenyewe hakuwepo kwenye tukio hilo kutokana na matatizo ya afya yake. Kwenye hafla hiyo, Rais Kikwete ametawazwa kuwa Mtemi wa Kabila la Wasukuma na amepewa jina la Ng’humbubanhu, jina ambalo lina maana ya “Mtu wa Watu, Kimbilio la Watu, Mwenye Upendo na Watu”. Kwenye halfa hiyo, mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete ametawazwa kuwa Mke wa Mtemi na kupewa jina la Mgole Mbula, jina ambalo lina maana ya malkia wa mvua. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM. 28 Novemba, 2013
Posted on: Sun, 01 Dec 2013 09:20:30 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015