Miaka Michache Ijayo Wakazi wa Namtumbo Wataangamia na Matokeo ya - TopicsExpress



          

Miaka Michache Ijayo Wakazi wa Namtumbo Wataangamia na Matokeo ya Urani..!! Hii siyo makala yangu ya kwanza kuhusu athari za machimbo ya urani hapa nchini, nimewahi kuandika makala kama hii miezi michache iliyopita nikaituma kwenye magazeti mbalimbali, lakini kwa bahati mbaya haikuwahi kuchapwa ila makala hiyo ipo kwenye Blog langu hili kwenye kurasa za mwanzo. Kwenye makala hiyo nilielezea athari mbalimbali zinazosababishwa na mieonzi ya madini haya ya urani (uranium) ambayo ni madini hatari sana kwa maisha ya binabamu, wanyama, viumbe na mimea kwa ujumla! Nisingependa kuyarudia yale yote ambayo yapo kwenye makala yangu hiyo ambayo pia inapatikana kwenye Blog hili, ila tu nilikuwa nataka kusisitiza kwamba Serikali ya CCM isifanye mzaha na maisha ya watanzania kwa vile madini haya ni hatari sana; tusifanye ushabiki wa kutafuta pesa tukasahau maana ya ubinadamu! Nimeshangaa kampuni ya Uranex inashabikia zoezi la kuendelea na mradi huo wa kuchimba madini hayo wakati tayari wananchi waliotumiwa kuchimba sample za madini hayo tayari wameshaanza kuathirika na mionzi ya madini hayo hatari kwa maisha ya binadamu na viumbe vyote kwa ujumla! Uranex wanajitetea eti walioathirika walikutwa wana ugonjwa wa kaswendwe! Kwani ukiathirika kwa mionzi ya urani huugui magonjwa mengine!? Mimi niliwahi kuishi kule Urusi kwa miaka mingi nchi ambayo ilitokea mlipuko wa mitambo ya Nuclear ijulikanayo kama “Chernobyl” mlipuko ambao uliitisa dunia nzima; mlipuko huo ulitokea miaka ya 1980s lakini hadi leo athari za mlipuko huo wa urani bado unaendelea kuitesa jamii ya Kirusi na utaendelea kwa karne nyingi zijazo! Naye mkuu wa kitengo cha Jiolojia cha chuo kikuu cha Dar es Salaam Dr. Shukuru Manya ambaye pia ni mtaalam wa madini hayo ya urani anasema kwamba madini ya urani yanayeyuka kwenye maji, hivyo ikigundulika kwamba maji hayo yana madini hayo, wananchi wasiyatumie kwa vile yana madhara makubwa! Dr. Shukuru Manya anatoa hoja kama vile yeye siyo Mtanzania na wala hajui hali halisi ya nchi yetu! Hivi mwananchi wa kule kijijini Mkuju ambapo madini haya yanachimbwa atajuaje kwamba maji hayo yameingia madini ya urani ikiwa hata hajui kusoma wala kuandika!? Mwananchi wa Mkuju atajuaje kama maji ya mto huo yamechanganyika na madini ya urani ikiwa hana elimu yoyote kuhusu madini yote kwa ujumla na wala hajui unani ni nini!? Mwananchi wa Mkuju atajuaje kwamba maji ya mto Mkuju yameingia madini ya urani ikiwa hana vipimo vya kupimia maji hayo!? Mwananchi wa Mkuju atajuaje kama mazao yake yameingia chembe chembechembe za mionzi ya urani!? Walaji wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine ambayo hunua bidhaa na mazao yanayozalishwa huko wilayani Namtumbo, watajuaje kama mazao hayo yana chembechembe za mionzi ya urani!? Mifugo na viumbe viishivyo wilayani Namtumbo vitagunduaje kwamba mazingira yao yameharibiwa na chembechembe za madini ya urani!? Pia ikumbukwe kwamba madini haya ya urani yanaweza kuwa kwenye maumbile ya vumbi (dust form) na kupeperushwa na upepo kutoka Namtumbo na kusambazwa naeneo ya wilaya za jirani na hata mikoa ya jirani bila ya kugundua kwa njia za kawaida, isipokuwa kwa kutumia vipimo vya kisasa ambavyo hatunavyo hapa nchini! Nilimtegemea Dr. Shukuru Manya atoe ushauri wa kuionya Serikali kusitisha mpango wake huo ambao ni hatari kwa taifa hili, lakini badala yake anatoa ushauri kama vile amekuwa mwanasiasa wa CCM!!! Ndugu zangu Watanzania Ufisadi utaliangamiza taifa hili miaka michache ijayo!!!! Kama Serikali itaendeleza ubabe wake wa tamaa wa kung’ang’ania kuyachimba madini haya ya urani kiholela kama dhahabu inavyochimbwa, basi kizazi cha watanzania kitaangamia kwa majanga na maradhi mbalimbali yanayotokana na madini haya! Pamoja na kwamba Dr. Shukuru Manya ni mtaalamu wa madini ya urani, lakini naamini hajawahi kuyashuhudia kwa macho yake madhara yaliyosababishwa na madini hayo, hasa kwa binadamu, wanyama, wadudu na mimea; naishauri Serikali imgharamie Dr. Shukuru Manya atembelee kijiji cha Chernobyl cha kule Ukraine – Urusi ya zamani ili ajionee mwenyewe, na nina uhakika akirudi atabadilisha ushauri wake kwa Serikali. Kule Urusi kuna kundi la watu wanaitwa “Chernobyl” yaani watu walioathirika kwa mlipuko huo ambao wengi wao wamelemaa, na watoto wanaozaliwa na watu wa jamii ya Chernobyl huwa si watoto wa kawaida bali ni watoto wenye viungo na sura tofauti na watoto wengine! Watoto hawa wengi wana viungo vya ajabu kama vile kuwa na macho matatu, au jicho moja, au masikio sita, vidole nane, pua ina matundu matatu au moja, au hawana nywele, au jicho moja kubwa na lingine dogo, au masikio yapo kwenye mashavu, au hawasikii, au hawaoni na mengine mengi ya kutisha! Watu wazima walioadhirika na mionzi ya urani ni kwamba ngozi yao inababuka na kuwa na magamba kama ngozi ya mamba, au wanaweza kuota manyama ya ajabu kwenye miili yao! Pia mionzi ya urani husababisha magonjwa ya kansa yenye sura za kila aina! Watu walioathirika kwa mionzi ya urani huwa ni vigumu kupata uzazi! Haya tukienda kwenye upande wa wanyama tutakuta ng’ombe anazaliwa ana vichwa vitatu na viguu sita na mengine mengi ya kutisha! Haya tukienda kwa upande wa wadudu napo utakuta wadudu wa ajabu wanazaliwa ambao hawapo popote pale duniani! Haya tukienda kwenye upande wa mimea, mimea yote hubadilika maumbile! Kwa mfano, mkorosho unaweza kugeuka na kuwa mwembe, na mwembe ukageuka ukawa mti pori usikuwa na jina na kadhalika! Kule nchini Russia watu wanaochimba madini ya urani ni wale wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha au waliohukumiwa kifo! Serikali ya huko inafahamu huwezi kuchimba madini ya urani halafu uishi zaidi ya miaka kumi! Haiwezekabni, ni lazima utakufa! Sasa sisi vijana wetu wazima wasiokuwa na hatia wanatumwa kwenda kuchimba madini ambayo yamewaletea madhara na hakika yameharakisha vifo vyao! Kwanini Serikali iruhusu vijana wazima wasiokuwa na hatia, na wala wasiokuwa wafungwa wa maisha wachimbe madini ya urani!? Je, kuna mtoto wa mkubwa yeyote anayechimba madini hayo ya kifo au ni watoto wa walalahoi? Mimi naiomba Serikali isitishe mara moja mpango wake huo wa kuchimba madini hayo ya urani hapa nchini kwa vile kuendelea na mpango huo ni kukiangamiza kizazi cha watanzania, hasa wananchi wa wilaya ya Namtumbo! Baada ya miaka 30 ijayo kizazi cha wakazi wa wilaya ya Namtumbo kitaangamia ikiwa ni pamoja na wanyama, wadudu na mimea wilaya hiyo! Wenzetu walioathirika kwa mionzi ya urani wa kule Urusi wanalipwa fidia na Serikali kwa kuwa na kitambulisho maalumu kinachowaruhusu kununua bidhaa kwa bei ya chini, kusafiri bure kwenye vyombo vyote vya usafiri vinavyomilikiwa na Serikali; wanasafiri kwa bei nusu klwa vyombo vya usafiri vya watu binafsi; wanapata matibabu bure kwenye hospitali zote za Serikali; wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Je, hapa kwetu Serikali imejipanga vipi kukabiliana na madhara ya mionzi ya urani!? Au Serikali inachojua ni kukazania kuchimba madini ya urani ili watawala na washirika wao wafaidi kwa kupata mapesa mengi na kuwaacha watanzania wakiangamia!? Tumefanya ufisadi mkubwa kwenye madini ya dhahabu, nisingependa tuendeleze ufisadi huo huo kwenye madini ya urani, hasa kwa vile madini haya yaweza kuifuta wilaya ya Namtumbo kwenye ramani ya Tanzania! Watawala wanaelewa madhara ya madini haya ya urani lakini wana tamaa ya utajiri wa haraka haraka licha ya kwamba ni matajiri wa siku nyingi, lakini wahenga wanasema “Tajiri hatosheki na pesa” kila anavyokuwa tajiri ndivyo anavyotaka aongeze utajiri wake! Nawaomba watawala wetu pamoja na Uranex kwamba wasifanye majaribio ya utajiri na maisha ya watanzania! Madini haya yapo nchi nyingi duniani, waende wakayachimbe huko nchi za mbali lakini siyo hapa nyumbani Tanzania. Nasema hivyo kwa vile sitaki kuona watu waliozaliwa wazima wakibadilika kwa kubabuka na kuota magamba kama ngozi ya mamba; sitaki kuona watoto wadogo wakizaliwa na vilema vya ajabu eti kwa vile watawala na Uranex wanataka utajiri wa haraka haraka! Kwanza naiomba Serikali ihakikishe kwamba inawafidia wale wote walioathirika na mionzi ya madini hayo ya urani kwa viwango vya kimataifa; na pia ihakikishe kwamba inasitisha mpango wake huo mara moja, mpaka hapo nchi itakapokuwa imejiandaa vya kutosha kifedha na kiteknolojia kuhusu uelewa wa madini hayo ya urani. Mwisho kabisa nawaomba waandishi wenzangu walivalie njuga swala hili la kupinga mpango huu wa Serikali ambao una hulka za kifisadi wa kutaka kuchimba madini ya urani sehemu mbalimbali hapa nchini, mpango huu una lengo la kukiangamiza kizazi cha watanzania muda si mrefu ujao..!!! noordinjella.livejournal
Posted on: Thu, 29 Aug 2013 18:56:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015